Tangazo la Coca Cola na ubunifu wake

Tangazo la Coca Cola na ubunifu wake

Mtoa mada ni MTU wa ajabu,unadhani kila MTU hilo tangazo analijua au kila MTU ana muda wa kushinda na tv?weka link au wimbo wenyewe.
Mmh hilo tangazo kweli hujawai liona?
 
Hili tangazo la Coca Cola 'Hey brother' limetengenezwa kwa ustadi na ubunifu mkubwa sana

Kwa kuanza tu wametumia soundtrack nzuri 'Hey Brother' ulioimbwa na kundi la Space Campa wakimshirikisha Josh Jones.
Huu wimbo hata mimi naupenda.

Angalia rangi za nguo, viatu na kofia walizovaa, headphones na ile game pad aliyoshika yule dogo; vyote hivyo vinashahabiana na brand ya Coca cola

Angalia vizuri pale kaka mtu aliyevalia kiatu cheusi akimkanyaga mdogo wake aliyevalia kiatu chekundu.Hapo kuna mantiki ya upinzani wa kibiashara.

Hawakuishia hapo, angalia tena pale kaka mtu alipokuja kumtetea mdogo wake tazama vizuri nguo na viatu walizovaa wale ma-bullies na zile walizovaa the two brothers kuna kitu hapo wanakiashiria.

Kweli biashara ni ubunifu
Sijalielewa mwisho baada ya brother kuisukuma chupa ya soda ikamwagika kidogo,lakini wakati anaondoka chupa ikaonekana imejaa
 
Mimi chakula kilikuwa hakipandi bila kuliangalia hivyo nililidowload kwenye simu yangu hapa nilipo pia naliangalia
 
Ilo tangazo nalipenda sana likifuatiwa na lile la Tigo pesa.

Pale mtoto anapoambiwa na mama sema mama huku baba yake akimwambia sema baba .....hahaha yeye kumbe yeye anatambua tu neno moja akasema NI TIGO PESA
Huwa nachekaga sana
 
Nikiliona tangazo hilo mda huo huo napata kiu ya kunywa soda bariidi.
 
Muda wa kuangalia tv ndio sina kabsa.
Unaagaliaga nini? Nikushauri kitu? Hivyo unavyohusudu kuviangalia wewe, huwa vinapofusha.
Tena wenzio huviagalia mara chache chache,ama kutoviangalia kabisa wakati wa kuvitumia.
Pendelea kuangalia tv. Tv ni salama kwa afya ya macho yako.
 
Mtoa mada ni MTU wa ajabu,unadhani kila MTU hilo tangazo analijua au kila MTU ana muda wa kushinda na tv?weka link au wimbo wenyewe.
Itakua poa kama utakua unaangalia tv kulivizia. Usipende miteremko
 
Back
Top Bottom