Ahsante Raia Mwema kwa kueleza huu ulaghai unaofanywa na Coca Cola. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ahsante Raia Mwema kwa kueleza huu ulaghai unaofanywa na Coca Cola.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kimbori, Sep 19, 2012.

 1. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,736
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Baada ya ‘kejeli’ hiyo ya mwaka 2008,
  kampuni hiyo hiyo ya vinywaji baridim
  mwaka huu imekuja na ‘kejeli’ nyingine,
  kumbuka wahenga walisema
  akutukanaye hakuchagulii tusi.

  Katika tangazo lao la wakati huu (tusi?)
  wamelibatiza jina la “Sababu Bilioni”, ni
  sababu bilioni za Waafrika kuendelea
  kutumia kinywaji cha Coca Cola. Wataalamu wa falsafa ya maana
  wanasema kwamba, maana ya neno
  haiko kwa mtamkaji bali kwa yule
  anayelipokea neno husika na kulitafsiri. Wewe ukishatamka neno, si kazi yako
  kueleza maana yake, bali msikilizaji.

  Tangazo la “Sababu bilioni” limeanza
  kwa kuwekwa nakshi na sifa ya maneno
  mengi mazuri na matamu kama vile
  nakupenda Afrika, mwanamke mzuri kuliko (sio mwenye elimu kuliko
  wanawake wote) anatoka Afrika, mwanaume mwenye mvuto kuliko wote
  (sio mwenye akili kuliko wote) anatoka
  Afrika, katika klabu zote bora za Ulaya
  kuna wachezaji bora kutoka Afrika, na
  vikorombwezo vyote na mbwembwe
  zote pamoja na mdundo mzuri wa muziki wa Kiafrika katika kupamba au
  kuburudisha tangazo husika.

  Lakini
  mwishoni mwa tangazo hilo ndipo penye
  tatizo ambalo limenikosesha raha hadi
  kuamua kuandika makala hii. Tatizo lipo kwenye maneno kwamba;
  “Wakati dunia inahangaika na majanga
  na kuhofia maisha ya baadaye, bilioni
  moja ya Waafrika wanakunywa na
  kufurahia Coca Cola.” Kwa kuzingatia wanafalsafa ya maana,
  tafsiri ninayoipata katika maneno hayo
  ni kwmaba, Waafrika bilioni moja
  hawajishughulishi kuhusu maisha ya
  baadaye. Kamwe hawana hofu na
  maisha ya baadaye.

  Waliotumika katika matangazo yale kwa
  asilimia kubwa ni Waafrika. Lakini sitaki
  kuamini kuwa waliofikiria kutengeneza
  matangazo yale ni Waafrika wenyewe. Nimechukua muda mrefu sana kutafakari
  maana ya tangazo hilo na hitimisho
  langu ni kwamba siku moja wahusika
  watatuomba radhi. Hizi kampuni za kigeni hata kama
  zinalipa kodi na kuajiri watu wetu
  katika biashara zao, lakini watumie
  namna nzuri ya kuendesha na kutangaza
  bidhaa zao.

  Ni kweli tunahitaji wawekezaji wa
  kigeni na wabia wengine wa biashara,
  lakini ukweli utabaki pale pale kuwa
  tunahitaji wabia katika biashara na
  wawekezaji ambao hadhi yetu kama
  binadamu inapewa nafasi ya kwanza. Natoa wito kwa Watanzania wenzangu
  na wote wenye kupenda heshima na utu
  wa binadamu kuwa sasa ni wasaa wa
  kampuni ya Coca Cola kuuomba radhi
  umma wa Waafrika kwa matangazo yao
  ambayo kwa namna fulani yamebeba tafsiri ya kudhalilisha utu wa Mwafrika
  na mtu mweusi kwa ujumla wake.
   
 2. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Ni sawa wenzetu wakati wanafikiria kwenda sayari ya Mars,sisi tunafikiria seminas,warsha na mambo mengine yasio na tija,wakati watu wanapiga kazi sisi tunalewa na kunjwa soda Coca cola wapo sahiii kabisa
   
 3. John locke

  John locke JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2012
  Joined: May 6, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 180
  Every 60 seconds in africa a minute pass.
   
 4. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,736
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Jinsi hilo tangazo lilivyo, inaonyesha ya kwamba, Waafrika tunasifiwa kwa upumbavu wetu wa kutofikiri juu ya maisha yajayo, bali tunakula na kunywa. Hii ni kejeli..
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  km mna uhakika wa kila siku jua kutoka asubuhi na kuzama jioni, kwa nini muwe na hofu? Sehemu yoyote yenye shida ndiko maendeleo yalipo. Nilipolisikia iliniuma lkn nilipokumbuka dhaifu na liwalo na liwe nikaona kweli
   
 6. S

  Samkyjr JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 364
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Yote ya juu ni uongo hilo la mwisho ndiyo sifa kweli ya sisi waafrika wenzetu wanafikilia wafanye nini sisi tunazunguka kuomba misaada.
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  mmewauuliza coca walikuwa na maana gani walipoweka hicho kipande au mnatoa tafsiri zenu?
   
 8. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,862
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Tangazo gani hili na ni la lini sijawahi lisikia... Coca sijanywa tokea 1989
   
 9. majany

  majany JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 30, 2008
  Messages: 1,199
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  well said....huwa nachela sana nikilisikia....bt LIWALO NA LIWE...
   
 10. peri

  peri JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  hivyo vinywaji nilisha viacha siku nyingi, mi yangu maziwa na maji.
  wajinga ndio waliwao.
  Ni waafrika wachache sana walio gundua kuwa hilo tangazo lina tatizo na haliko sawa. Wengi wamedndelea kufurahia na kunywa cocacola.
   
 11. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #11
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,335
  Likes Received: 2,659
  Trophy Points: 280
  lile tangazo limeficha ujumbe wa Illuminati...hawa jamaa wamekuwa na kawaida ya kutoa cautions kabla ya tukio kubwa linalogharimu maisha ya wengi...
  Kuna mtu hapa amenote maneno "The End is Near" mwishoni kabisa mwa lile tangazo? if the answer is yes the stop taking cola drinks.
   
 12. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #12
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,808
  Likes Received: 2,583
  Trophy Points: 280
  The statement "while the rest of the world is busy worrying about future, one billions Africans are busy enjoying a coca cola" simply means while rest of world is worrying about economic reccession Africa is enjoying unprecedented growth. Ndugu relax have a Coke.
   
 13. John locke

  John locke JF-Expert Member

  #13
  Sep 20, 2012
  Joined: May 6, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 180
  Mkuu upo North Korea au Cuba? Kwa sababu ndiyo sehemu pekee ambazo Coca cola haipatikani.
   
 14. j

  jaffery hassan Member

  #14
  Sep 20, 2012
  Joined: Dec 9, 2008
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  waafrica tunadharaulika............mh nilikuwa napita tu,but thanks kwa ufafanuzi
   
 15. nziriye

  nziriye JF-Expert Member

  #15
  Sep 20, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 960
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  lakini tukumbuke hilo tangazo halikutengenezwa kwa maana ya kvusanifu watanzania kwani naona most of comments kama zinaonyesha sisi watanzania ndo tumeonewa,tukumbuke bara la afrika lina nchi zaidi ya 50 so its the task of all countries kuamka na kushirikiana kulipinga.
   
 16. Bwana Mapesa

  Bwana Mapesa JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,925
  Likes Received: 660
  Trophy Points: 280
  this z what we call "critical thinking".Heshima kwako mkuu..
   
 17. +255

  +255 JF-Expert Member

  #17
  Sep 20, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,908
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Soma tena hiyo makala. Mwandishi amesema kabisa maana ya neno haipo kwa mtamkaji ila ipo kwa yule anayelipokea neno.
   
 18. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #18
  Sep 20, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nafikiri tatizo hapa liko kwenye hiyo dharau yao lakini Coca Cola kama kinywaji hata Ulaya wanainywa kwa sana tu.
   
 19. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #19
  Sep 20, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Safi coca cola wanatupatia vinywaji safi ajira kwetu na misaada kwa jamii
   
 20. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #20
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sababu Bilioni ........... ni pamoja na uongozi mbovu ktk serikali nyingi za kiafrika
   
Loading...