Tangazo la ajira Polisi

paesulta

JF-Expert Member
Mar 13, 2009
227
29
TANGAZO LA AJIRA
Jeshi la Polisi liko katika mchakato wa kuajiri vijana kujiunga na Jeshi kupitia mashuleni.
Tumeamua kuurudia utaratibu ambao ulikuwepo zamani wa kuajiri moja kwa moja toka mashuleni ambao ulikuwepo siku za nyuma kutokana na mahitaji halisi ya Jeshi la Polisi kwa sasa.
Hivi sasa Jeshi la Polisi linakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazotokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, ongezeko la uhalifu mpya kama vile wizi wa kutumia mtandao, usafirishaji haramu wa binadamu na kadhalika. Wahalifu wanaohusika na matukio kama hayo, wamekuwa wakitumia mbinu mpya na utaalamu wa hali ya juu.
Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea na Programu yake ya maboresho. Maboresho haya yanalenga kulifanya Jeshi kuwa la Kisasa zaidi ambalo litatelekeza majukumu yake kwa Weledi huku likiwa karibu zaidi na raia katika utendaji wake wa kila siku.
Kutokana na changamoto hizo, Jeshi la Polisi linahitaji kuajiri, vijana wasomi, wenye utashi, ari na nia ya kufanya kazi za Polisi na wenye fikra na mtazamo unaoendana na dunia ya sasa.
Vijana hawa watakuwa viongozi na chachu katika kuleta mabadiliko yanayokusudiwa ndani ya Jeshi la Polisi.

A: – SIFA/VIGEZO VYA MWOMBAJI
Mwombaji awe Mtanzania kwa kuzaliwa.
Awe na afya njema iliyothibitishwa na Daktari wa Serikali.
Awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto.
Awe na tabia njema na asiwe na kumbukumbu za uhalifu.
Awe amemaliza Kidato cha sita mwaka 2012 na kufaulu.
Awe na umri kati ya miaka 18 na 25.
B: MASHARTI KWA MWOMBAJI
Kila mwombaji awe tayari kufanya kazi mahali popote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kila mwombaji awe na ari,utashi na nia ya kufanya kazi ya Polisi.
Kila mwombaji aandike namba yake ya simu na anuani yake ya kudumu kwa usahihi ambayo itatumika wakati wa kuitwa kwenye usaili.
C: FOMU ZA KUJIUNGA ZINAPATIKANA:
Ofisi ya Mkuu wa shule
Ofisi za Makamanda wa Polisi Mikoa/Wilaya zilizo karibu
Pata fomu hapa(sel-form) SEL-FORM

Imetolewa na;
Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P 9141,
DAR ES SALAAM.
Source: TANGAZO LA AJIRA B 2012
 
haya vijana nafasi ya kujenga nchi na kusimamia ustawi bora wa jamii yetu ndiyo hii..tujifunge mkanda sasa
 
Ina maana ni fom 6 tu ndo wanaopaswa kuomba hzo nafasi? Vp wanavyuo na waliomaliza form 4.?
 
Why usiwe na mtoto au hujaona au kuolewa hizi ajira sasa zinakuwa discriminatory( za kibaguzi) na ni kinyume cha katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania
 
Hunidanganyi nikapoteze muda wa kuwa police wa kutumwa niwapige watu wanaodai haki zao kwa faida ya wanasiasa. Labda kama kuanda jeshi la waasi naweza kuhamasika kwani najua through hao tutapata kuikomboa TZ
 
TANGAZO LA AJIRA
Jeshi la Polisi liko katika mchakato wa kuajiri vijana kujiunga na Jeshi kupitia mashuleni.
Tumeamua kuurudia utaratibu ambao ulikuwepo zamani wa kuajiri moja kwa moja toka mashuleni ambao ulikuwepo siku za nyuma kutokana na mahitaji halisi ya Jeshi la Polisi kwa sasa.
Hivi sasa Jeshi la Polisi linakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazotokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, ongezeko la uhalifu mpya kama vile wizi wa kutumia mtandao, usafirishaji haramu wa binadamu na kadhalika. Wahalifu wanaohusika na matukio kama hayo, wamekuwa wakitumia mbinu mpya na utaalamu wa hali ya juu.
Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea na Programu yake ya maboresho. Maboresho haya yanalenga kulifanya Jeshi kuwa la Kisasa zaidi ambalo litatelekeza majukumu yake kwa Weledi huku likiwa karibu zaidi na raia katika utendaji wake wa kila siku.
Kutokana na changamoto hizo, Jeshi la Polisi linahitaji kuajiri, vijana wasomi, wenye utashi, ari na nia ya kufanya kazi za Polisi na wenye fikra na mtazamo unaoendana na dunia ya sasa.
Vijana hawa watakuwa viongozi na chachu katika kuleta mabadiliko yanayokusudiwa ndani ya Jeshi la Polisi.

A: – SIFA/VIGEZO VYA MWOMBAJI
Mwombaji awe Mtanzania kwa kuzaliwa.
Awe na afya njema iliyothibitishwa na Daktari wa Serikali.
Awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto.
Awe na tabia njema na asiwe na kumbukumbu za uhalifu.
Awe amemaliza Kidato cha sita mwaka 2012 na kufaulu.
Awe na umri kati ya miaka 18 na 25.
B: MASHARTI KWA MWOMBAJI
Kila mwombaji awe tayari kufanya kazi mahali popote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kila mwombaji awe na ari,utashi na nia ya kufanya kazi ya Polisi.
Kila mwombaji aandike namba yake ya simu na anuani yake ya kudumu kwa usahihi ambayo itatumika wakati wa kuitwa kwenye usaili.
C: FOMU ZA KUJIUNGA ZINAPATIKANA:
Ofisi ya Mkuu wa shule
Ofisi za Makamanda wa Polisi Mikoa/Wilaya zilizo karibu
Pata fomu hapa(sel-form) SEL-FORM

Imetolewa na;
Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P 9141,
DAR ES SALAAM.
Source: TANGAZO LA AJIRA B 2012

matokeo ya form six yatatoka mwezi may,wakati tangazo litakuwa limepitwa na wakati.
 
Nami pia lilinishangaza hilo,lkn anaetaka jaribu bahati na ajaribu,au kama kuna vijana tunawajua na wanataka upolisi,basi tuwajuze.
 
Huo utaratibu mpya wa ku recruit vijana fresh from school umeletwa kwa sababu freshers wengi wanakuwa bado hawajawa exposed na mambo ya kiharifu tofauti na wakimchukua mtu aliyemaliza miaka ya nyuma baada ya kuangaika sana na maisha ndo anaona polisi ndo kimbilio lake, wanataka wafute hii altitude
 
kazi kwenu vijana wa Tanzania wenye sifa,jaribuni fursa kuliko kuendelea kukaa vijiweni.
 
Huo utaratibu mpya wa ku recruit vijana fresh from school umeletwa kwa sababu freshers wengi wanakuwa bado hawajawa exposed na mambo ya kiharifu tofauti na wakimchukua mtu aliyemaliza miaka ya nyuma baada ya kuangaika sana na maisha ndo anaona polisi ndo kimbilio lake, wanataka wafute hii altitude

pia wamegundua mtu akikaa bila kazi muda mrefu ndio mwanza wa kujaribu kughushi vyeti ili apunguze umri.
 
Polisi makao makuu vp? Mngewasiliana na wizara ya Elimu kama wamesha toa matokeo ya kidato cha sita kuliko kukurupuka hivi
 
Wanataka wawatumie kisiasa vijana wawe wanapiga watu kwa manufaa yao pale ambapo wananchi wanapodai haki zao kimsingi,kwanza vijana hao wanatakiwa waendelee na masomo yao ya juu,pia nawahamasisha vijana wote wa Tanzania kutojiunga na ****** huo,ni bora wasubiri si muda mrefu tutapoanzisha jeshi la uasi la kuikomboa Tanzania kutoka kwa wanyang'anyi mafisadi.
 
Yani mtu afaulu vzr afu aende upolice?hao labda wanataka failures
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom