Tangazo la ajira bomba la mafuta Tanzania - Uganda

TangataUnyakeWasu

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
1,269
1,585
TAARIFA KWA UMMA

KUTAMBUA WATANZANIA WENYE TAALUMA NA UJUZI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI

1. Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi “East Africa Crude Oil Pipeline (EACOP)” kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani, Tanga nchini Tanzania ni moja ya miradi mikubwa kutekelezwa hapa nchini ambao unategemea kugharimu Dola za Kimarekani 3.5 Billioni sawa na shillingi Trillion 8 za Kitanzania. Bomba hilo linategemewa kuwa na urefu wa kilometa 1,445 ambapo ujenzi wa kilometa 1,115 za bomba hilo utafanyika nchini Tanzania. Jumla ya wilaya 24 na vijiji 184 hapa nchini vinategemewa kupitiwa na bomba hilo katika mikoa 8 ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga.

2. Mradi huo ambao ujenzi wake unatarajiwa kuchukua kati ya miezi 24 hadi 36, unategemewa kuzalisha fursa za ajira takriban 10,000 wakati wa ujenzi na ajira zaidi ya 1,000 wakati wa uendeshaji wake. Hivyo, ili kuhakikisha kwamba Watanzania wengi wananufaika na fursa za ajira zitakazotokana na mradi huo, Wakala unapenda kuwahamasisha Watanzania wote wenye taaluma na ujuzi katika Sekta ya Mafuta na Gesi kujisajili TaESA ili waweze kuingizwa kwenye kanzidata ya Wakala kwa lengo la kuiwezesha Serikali kubaini idadi halisi ya Watanzania walio na sifa zinazohitajika na walio tayari kuajiriwa kwenye mradi huo.

3. Zoezi la usajili limekwishaanza na linatarajiwa kukamilika tarehe 30/03/2018. Usajili huu unafanyika kwa kujaza fomu maalum inayopatikana kupitia tovuti ya Wakala ya www.taesa.go.tz au kwa kufika kwenye ofisi zetu za kanda zilizoko Dar es Salaam, Arusha, Dodoma na Mwanza. Fomu zilizojazwa zinaweza kuwasilishwa kwenye ofisi zetu za kanda au kwa barua pepe: eacop@taesa.go.tz. Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kupitia namba zifuatazo: 0736 551 055; 0739 221 022; 0735 221 022; 0735 551 055 na 0282 541 840/1.

IMETOLEWA NA:
KAIMU MTENDAJI MKUU
WAKALA WA HUDUMA ZA AJIRA TANZANIA
 
46fb9e77-a422-4aa4-916d-1575f6ee11f4.jpg
 
Samahani anae fahamu office za TAESA katika mkoa wa mwanza ziliko anisaidie
 
hivi michakato imeshaanza huko, watu tunataka tukatie kambi tupige hata biashara ya kuwauzia chakula cuz kazi itakuwa ngumu kupata
Walianzaga muda sana hawa jamaa, naona labda ni batch nyengine hii!
 
Back
Top Bottom