Tangazo kwa vijana wote wenye fikra za kimapinduzi ambao bado wako magamba! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tangazo kwa vijana wote wenye fikra za kimapinduzi ambao bado wako magamba!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chaimaharage, Apr 18, 2012.

 1. Chaimaharage

  Chaimaharage JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baragumu limepigwa, chukueni maamuzi wale wote walio na fikra za kimapinduzi ambao mpaka sasa bado mnasita kuamua kutokana na hofu ya kufitiniwa na magamba wakisaidiwa na vyombo vyao vya dola ambapo mwanzo vilikuwa polisi na jeshi, hivi karibuni Mahakama imejiunga rasmi na magamba kwa kufanya maamuzi ambayo kila mtu ameyaona na tutaendelea kuyaona.Muda si mrefu tutaiita mahakama ya magamba ikiongozwa na majaji wa magamba.Tuna subiri maamuzi ya rufaa ya Lema tilithibitishe hili kwa sababu hata kilaza wa sheria ile kesi isinge msumbua. Huko mbeleni itabidi maamuzi yenye mustakabali wa nchi tuyafanye wenyewe kama wenzetu Mali, Guinea Bissau na kwingineko walio thubutu.

  Sasa basi James Millya amefungua milango, hapa ndipo tutawajua wana harakati wa ukweli ndani ya magamba. Huwezi kufanya harakati kwa kusafiri na meli inayozama. Nadhani Mh.Deo Filikunjombe na Mh.Samuel Sitta mnanielewa. Mnacho kifanya mkiwa ndani ya magamba ni kiini macho, hatuwaelewi. Mnataka kutuambia kuwa kwa kelele zenu mnaweza kubadili sera mbovu kuwa nzuri na za matumaini? mafisadi washughulikiwe inakuwa kama vile wajishughulikie wenyewe kwa sababu fuvu tupu au kichwa cha nazi kilichoko magogoni ni tape root/ fisadi papa. Hivyo basi angalau mfanye hivyo mkiwa kwingine siyo lazima iwe CDM ili tuwaone kweli mko serious.

  Hamuwezi kushinda vita yenu mkiwa na raisi yule yule(kichwa cha nazi), mawaziri wale wale vichwa vya nazi, na wabunge kibao wa magamba vichwa vya nazi. Hapa namtaja mmoja wengine mtamalizia; Livingstone(now dead stone) Lusinde.

  Kuna vijana ambao bado wana safari ndefu katika midani za siasa kama vile Nape, January Makamba na wengine lakini bado hawaoni kuwa CCM inakufa hata wazee wao wametabiri. Leo jamvini kuna mtu ame post thread inasema Nape ni kama waziri wa zamani wa Iraq. Jamaa alikuwa bingwa wa propaganda akisema "wamarekani tunawapiga na tutashinda vita", nadhani mwisho wake sote tunaujua. Kumbukeni Nape alisema "Arumeru tutashinda kwa kishindo" yuko wapi? Yaani ukiangalia unaona future yao katika siasa ni vague au uncertain. Ndiyo maana kuna mtu humu jamvini alisema "unahitaji kuwa na akili ya maiti kuishabikia sisiemu, huu ni ukweli usio pingika".
   
 2. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nape bada haamini kinachotokea CCM, na Sitta anaoma aibu tu kuondoka, lakini hana analolifanya ccm ambalo litaibadilisha ccm kwa muda huu. Hakuna muokozi wa kuiokoa ccm kwa muda ulibaki. Nakumbuka wakati JK anaingia kwa kishindo madarakani mwaka 2005 makanisa na misikiti wakasema kuwa ni mteule wa Mungu...sijui Mungu gani? But now I believe TRUELY that ni kweli JK ni mteule wa Mungu, aliyetumwa kuja KUIMALIZA CCM....Hili liko wazi na anayepinga ni mbishi tu, lakini ukweli unabaki kuwa JK anaondoka na CCM, na kama wakitaka kulazisha ccm kuwa madarakani, tutafanya ambayo hayajawahi kufanywa hapa duniani na kisiwa cha amani kitageuka MACHINJIO.....Mungu atuepushe na haya, but if there is no way...TUTAFANYA HIVYO KWA AJILI YA NCHI YETU NA WATOTO WETU.....

  TOGETHER WE CAN BRING THE CHANGES WE NEED....YES WE CAN.....GOG BLESS CDM.....AND ALL OF US....
   
 3. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  sita,mwaakyembe wote ni wanachadema hawana mpango na ccm
   
 4. K

  KAFWIMBI Member

  #4
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika vita huwa wapo raia au hata askari wa upande wa adui wanaopigana vita "against" nchi yao. Hawa wanafaida zake kutuletea habari za namna bora ya kuvishinda vita tunavyopigana, si lazima wote waje huku au wajitokeze hadharani kama MILLYA.........Hao walioko huko na kutenda kazi zao kwa uaminifu kwa CDM hao ni wapenda maendeleo hatuna budi kuwatia moyo..........ndo maana hata taarifa nyeti kama hukumu ya Mh. Lema ilipatika hata kabla jaji hajaisoma long live wote walio "LOYO" kwa CDM na kuchagiza maslahi ya umma
   
Loading...