Jana watu walitilia shaka hii kitu ya TCU. Kuna vyuo vilivyopotea (KIU, AJUCO, MARIAN etc) na programs ambazo zamani zilitotelewa na vyuo lakini sasa havionekani. Swali kulikuwa na makosa au ndo maamuzi ya TCU. Ilitakiwa TCU kwenye lile andiko lake la Program zilizo kuwa approved kuwe na utangulizi ili waombaji wasije wakaingia mkenge. Ukienda kwenye website unakuta course/program imetangazwa na chuo ukienda TCU document hiyo kiti haipo. Kwa namna hii TCU inachanganya waombaji. Hivyo wanatakiwa wa withdraw ile document na watoe document yenye utangulizi ku-direct watu kwamba kilicho nje ya kitabu cha TCU hakikubaliki au vinginevyo. Mwisho wa yote walio toa jana si guide book walitupa list ya vyuo na approved programmes bila maelekezo yeyote.