Tanganyika - Liemba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanganyika - Liemba

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Kipala, Apr 20, 2010.

 1. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,536
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Waheshimiwa, nina maswali mawili kuhusu ziwa Tanganyika na jina lake.

  a) Yuko anayejua maana asilia ya neno "Tanganyika"?

  Nilisikia ni TANGA (=la jahazi) + NYIKA (=pori).
  Nina wasiwasi sana kwa sababu
  # sielewi maana ya jina hili kama ni kweli
  # sijaona habari ya uhakika kuwa jina lenyewe ni la Kiswahili - labda limetoka katika lugha nyingine na kuswahilishwa?

  b) Je ni kweli "Liemba" ilikuwa jina la sehemu ya kusini ya ziwa Tanganyika kwa Kifipa?
  Nilichungulia online kwa David Livingstone lakini sipati picha kamili - ama ni ziwa lenyewe au jina kwa eneo upande wa kusini wa ziwa au ni watu ?
   
Loading...