TANGANYIKA LAW(less) SOCIETY | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANGANYIKA LAW(less) SOCIETY

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mwanamasala, Dec 15, 2009.

 1. m

  mwanamasala JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2009
  Joined: Jun 20, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tanganyika Law Society,sasa naiita Lawless Society ni institution ya zamani sana toka tupate uhuru.Baadhi ya members wake wametia aibu katika fani hii hasa hapa Tanzania.Imeonekana ni fani ya corruption ,haisaidii mtu mnyonge wa huko kijijini au mwananchi wa kawaida.
  Angalieni watu hawa na scandal zao:
  1.Mkono&Advocate-Maozo ya BOT ya kulipwa zaidi ya Tshs 8billion
  2.Malegesi Law Chambers-Kulipwa zaidi ya Tshs 40 billioni za EPA
  3.Lawrence Masha-Scandal ya vitambulisho(ID)
  Baadhi ya hawa ni lawmakers(wabunge) bila ya kumsahau baba yao myantuzu Bw Chenge ambaye alikutwa na £500000/=kwenye offshore account!

  Hawa wote ni wanachama wa Tanganyika Law Society.Unajiuliza je,
  kuna Ethics katika Society hii?Ingekuwa nchi ya sheria hawa wote
  wangekuwa wamefutwa na kunyanganywa leseni ya kupractise!
  Lakini Tanzania wanapeta na hawashikiki.

  Fani ya usheria Tanzania ni a joke now!Waone akina Lamwai,Marando walivyodisgrace upinzani.Labda wanaJF mnajua lawyers ambao wanafanya kazi kwa manufaa ya nchi!I guess ni wachache sana.My favourite lawyers of all time Tanzania ni:
  1.Judge James Mwalusanya
  2.Tindu Lissu.
  Taja wakwako
   
 2. KILITIME

  KILITIME JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kweli, unategemea nini kama watuhumiwa ndio wameshikilia usukani? Usisahau Chenge yuko NEC (Policy maker), Bungeni (Lawmaker) na zamani alikuwa Waziri (Law enforcer)! Sasa hapo unategemea nini?
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ma lawyers walikuwepo kina Judge Nyalali, waliokuwa wanamfundisha Nyerere kuhusu separation of Judiciary and Executive.

  Siku hizi watu wana njaa tu.. Nasikia Jaji Makame anaahidi uchaguzi huru na wa haki, hata haogopi mzimu wa 95 na uchafu waliomfanyia Seif, yeye na swahiba wake Nyerere aliyefanya mchezo wote!
   
 4. m

  mwanamasala JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2009
  Joined: Jun 20, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Jaji Makame a joke of all time.Huyu anakula pesa za taxpayers too.1995 election fiasco tunaikumbuka sana.Hawa ni status quo!Ndio wanajiita lawyers wa kibongo.
   
 5. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2009
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  The President Dr. Fauz Twalib of TLS has let down the society! He has been in deep slumber even in big issues of national interest; absurdly, one of his last engagements according to his own diary on the TLS website was in Feb 2009 ( so long!) and in fact, it reads like "The President missed his return flight to Dar es Salaam after some immigration mishaps at Oliver Tambo International..." I suppose from one of these useless conferences (sheer absurdity)
  It is an undeniable fact that TLS has joined the order of many Tanzania NGOs and Institutions namely being just the forums for useless seminars, conferences, anniversaries, which bear no fruits in the life of Tanzanians but simply ways of collecting sitting allowances!
  All these cases of the national interest such as EPA, IDs' scandal, Radar issue etc have not awaken the deep slumber of Dr. Fauz Twalib! We have not even heard a comment from the TLS President about these issues, leave alone intervention in offering legal assistance or advocacy for the people of TZ ! Make a soul searching exercise TLS' members and your honorable President!
   
 6. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  DU, Sasa kama rais na serikali nzima including TAKUKURU wanaponda nchi, why not wao? hii nchi haina mwenyewe, wewe popote ulipo jitahidi upate chako na familia yako.
   
 7. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #7
  Dec 17, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,085
  Likes Received: 24,102
  Trophy Points: 280
  HOTUBA YA DR. FAUZ TWAIB, RAIS WA CHAMA CHA MAWAKILI WA TANGANYIKA (TLS)
  KATIKA HAFLA YA KUWAKUBALI WA KUWASAJILI MAWAKILI WAPYA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA, DAR ES SALAAM
  TAREHE 15 DESEMBA 2009

  Mheshimiwa Jaji Mkuu, Augustino Ramadhani,
  Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania,
  Mheshimiwa Jaji Kiongozi Fakih Jundu,
  Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania,
  Mheshimiwa Frederick Werema, Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
  Waheshimiwa Wasajili wa Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu,
  Waheshimiwa mahakimu
  Marafiki wasomi, mawakili wenzangu (binafsi na wa Serikali) mliohudhuria hapa,
  Marafiki wasomi, mawakili wapya mnaosajiliwa leo,
  Wageni Waalikwa,
  Mabibi na Mabwana,

  Leo hii tunawakaribisha mawakili wapya 55 katika utume wa taaluma ya uwakili. Siku zote ni furaha kwangu kuona idadi ya mawakili ikiongezeka. Kama kiongozi mkuu wa TLS, nasema karibuni sana mawakili wapya katika fani yetu hii. Nina hakika kuwa damu na mawazo yenu machanga yataotupa chachu ya kuboresha shughuli za Chama chetu na fani yetu katika kuhudumia umma wa Watanzania.

  Ni matumaini yangu kuwa mtatumia muda na ujuzi wenu wa uwakili vizuri na kwa ueledi unaostahili kama wenzenu waliowatangulia, na kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za Chama chetu zilizoko mbele yetu.

  Mheshimiwa Jaji Mkuu,
  Nisingependa kuwa kama muazima jamvi aliyechelewa kuelezea shida yake kwa kunogewa na ngoma hata akasahau sababu iliyompeleka pale. Ni bora niende moja kwa moja kwenye maudhui niliyokusudia kuyasema.


  Mheshimiwa Jaji Mkuu,
  Nchi yetu inakabiliwa na uhaba mkubwa wa wataalamu wa sheria, wakiwemo mawakili. Kwa takwimu zilizopo, idadi ya mawakili walio katika orodha ya mawakili (Roll of Advocates), ukiondoa hawa waliopata uwakili leo, ni 1165. Kati ya hao mawakili wanaofanya kazi hasa ya uwakili hawafiki 800 kwa nchi nzima. Ni dhahiri kuwa idadi hii ni ndogo sana na haitoshelezi mahitaji ya wananchi wetu wanaokaribia milioni 40. Wenzetu wa Kenya wana mawakili zaidi ya 7,000 wakati Uganda wana zaidi ya 2,000. Idadi hii inaongezeka kwa kasi maradufu ukilinganisha na hapa kwetu Tanzania.

  Kwa kuwa sasa tunaelekea kwenye mfumo ambao utaruhusu mawakili wa nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki kufanya kazi katika nchi nyingine yoyote iliyo mwanachama, kuna haja kubwa ya kuhakikisha kwamba tunawaongezea wanasheria Watanzania uwezo wa kutosha kukabiliana na ushindani huu. Njia mojawapo ya kufanya hivyo kama taifa ni kuwapa wananchi wenzetu walio wanasheria, na hasa wale wanaosubisi kusailiwa na kusajiliwa kama mawakili, nafasi ya kupiga angalau hatua moja mbele kwa kujiunga na fani hii, kabla ya mipaka haijafunguliwa kabisa na kuacha nafasi zilizopo kuangukia mikononi mwa majirani zetu. Kama wasemavyo Waingereza, "charity begins at home".

  Mheshimiwa Jaji Mkuu,
  Wakati tuna tatizo hili kubwa la uhaba wa wanasheria na hasa mawakili, kwa sasa kuna maombi (petitions) 1714 ya wanasheria wanaohitaji kusajiliwa kama mawakili kwa kupitia mfumo wa zamani wa Baraza la Elimu ya Sheria (Council of Legal Education). Vilevile, kuna maombi 55 ya wanafunzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (Law School of Tanzania) ambao wamekidhi vigezo vya kupata uwakili vilivyowekwa na sheria iliyoanzisha Taasisi hiyo, yaani Law School of Tanzania Act. Hakika hii ni idadi kubwa sana ya wanasheria ambao wanaweza kupata usajili na kuanza kazi mara moja.

  Mheshimiwa Jaji Mkuu,
  Ni vizuri tukubali kuwa mfumo uliopo sasa wa kutahini wanasheria wanaoomba kuwa mawakili kwa usaili wa Baraza la Elimu ya Sheria unahitaji kuangaliwa upya. Hatuna budi kufanya juhudi za makusudi kurekebisha hali hii. Naamini inawezekana.

  Kwa kuzingatia haya, hapo jana nilituma kwako, Mheshimiwa Jaji Mkuu, waraka wenye mapendekezo ya Chama chetu. Ni matumaini yangu kuwa waraka wangu umeupata na utaufanyia kazi mapema iwezekanavyo. Ninaamini kuwa kama mapendekezo niliyoyatoa yatakubaliwa, sherehe ijayo ya kuwaapisha mawakili huenda ikawa na idadi ya mawakili hata 500 watakaosajiliwa kwa mara moja. Pengine itabidi tuanze kufikiria sehemu kubwa zaidi wa kufanya shughuli hii zaidi ya hapa tulipo.

  Mheshimiwa Jaji Mkuu,
  Nitakuwa mchoyo wa fadhila iwapo sitaongelea uhusiano mzuri uliopo kati ya Chama chetu, kwa upande mmoja, wewe binafsi, ofisi yako na Mahakama kwa ujumla kwa upande mwingine. Kama ulivyoahidi huko nyuma, ofisi yako imekuwa wazi kwetu wakati wote. Umekuwa tayari kushirikiana nasi katika mambo mengi, hata pale tulipokuletea taarifa ya muda mfupi.

  Kwa niaba ya wanachama wote wa TLS, nashukuru kwa kukubali kwako kuja kufungua mkutano wetu wa Nusu Mwaka mwezi Agosti pale Mlimani City. Tulifarijika sana. Tulifarijika zaidi tulipoona kuwa uliongozona na majaji zaidi ya wanane (8) kutoka Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu. Sikumbuki kama TLS tulishawahi kuwa na mkutano uliohudhuriwa na majaji wengi kama vile. Tunashukuru sana, na tunawashukuru majaji wote waliohudhuria siku ile. Moyo huu wa ushirikiano uendelee kwa faida ya taasisi zetu, taaluma yetu ya uanasheria, mfumo wetu wa utoaji haki, na jamii nzima ya Watanzania.

  Tunashukuru pia kwa invitation to treat uliyotupa, iliyofuatiwa na offer kamili ambayo tuliipokea kwa mikono miwili, kwa TLS kuhudhuria mkutano wa majaji uliofanyika Arusha ambapo mimi na Makamu wangu, Bw. Felix Kibodya, tulihudhuria. Ilikuwa heshima kubwa kwangu kama kiongozi wa Mawakili uliponipa nafasi ya kusema machache mbele ya hadhara ya waheshimiwa Majaji wa Tanzania nzima na kubadilishana nao mawazo.  Mheshimiwa Jaji Mkuu,
  Ningependa kuchukua fursa hii kuwajulisha waliohudhuria hapa mambo machache kuhusu shughuli za TLS mwaka huu, ambayo yameonyesha mafanikio.

  Jambo la kwanza ni kuhusu utaratibu wa lazima wa mawakili kujiendeleza katika taaluma yao, yaani Mandatory Continuing Legal Education. Utaratibu huu, ulioanza rasmi mwaka huu, umekuwa wa mafanikio sana. Mawakili wengi wameitikia wito na wamehudhuria mafunzo mbalimbali yaliyotolewa ndani na nje ya nchi yetu. Sisi kama chama tuliweza kuandaa zaidi ya semina 15 katika mikoa mbalimbali ya Tanzania kwa ajili ya kuwapa mawakili ujuzi mpya wa sheria mbalimbali. Tulijatahidi, pale uwezo uliporuhusu, kuwaalika baadhi wa watendaji wa mahakama na kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili nao wapate nafasi ya kupata mafunzo hayo.

  Nina furaha kukujulisha kuwa utaratibu huu umekuwa wenye mafanikio na uliopokelewa vizuri na mawakili wengi, ingawa bado kuna mawakili wachache ambao hawajaona faida ya utaratibu huu. Tunaamini kwamba jinsi siku zinavyosonga mbele, wenzetu hawa pia wataona faida ya CLE.

  Jambo la pili ambalo ningependa kulielezea leo ni kuhusu utoaji wa msaada wa sheria. Chama chetu kimeendelea kutoa msaada wa bure wa sheria kwa watu wasio na uwezo. Ni jambo la kufurahisha tunapoona na kutambua kuwa hata idara ya mahakama imetambua mchango wetu na mara nyingi imekuwa ikiwalekeza wateja waje kwetu. Tunatoa shukrani kwa ushiriakiano wenu.

  Vilevile mwaka huu tuliadhimisha tena Siku ya Msaada wa Sheria, yaani "Legal Aid Day". Tuliadhimisha siku hii katika Mikoa 8 ya Tanzania bara, ambayo ni Mtwara, Lindi, Manyara, Mara, Ruvuma, Rukwa, Kagera, Singida, Kigoma na Dar Es Salaam. Kitaifa, siku hii iliadhimishwa Mtwara, ambako mgeni wetu rasmi alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Mathias Chikawe.

  Ukiangalia mikoa tuliyoadhimisha mwaka huu utagundua kuwa tulichagua mikoa ambayo (ukiondoa Dar s Salaam) huduma za mawakili ama hazipo kabisa na kama zipo, basi mawakili waliopo hawazidi wawili.

  Katika kuadhimisha siku hii tumejifunza mambo mengi lakini kubwa zaidi ni kwamba wananchi wengi wana matatizo na wanahitaji msaada wa sheria. Wapo watu ambao wana uhitaji wa huduma hiyo hata kwa kulipia gharama ndogo, lakini hakuna mawakili.

  Mheshimiwa Jaji Mkuu,
  Ni dhahiri kwa hali hii ya uhitaji wa huduma za wanasheria, ombi langu kuhusu utaratibu wa kuwasaili mawakili niliouzungumzia awali litakuwa na maana zaidi. Kuongezeka kwa mawakili kutasaidia sana kutawanya mawakili katika sehemu ambazo kwa sasa hazina huduma hiyo kabisa, na pia kutasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za huduma za mawakili, ambazo ni mojawapo ya changamoto kuu zinazokabili utoaji wa haki kwa wananchi wasio na uwezo wa kulipia gharama za uwakili.

  Mheshimiwa Jaji Mkuu,
  Kabla sijahitimisha hotuba yangu hii, naomba niseme machache kwa mawakili wapya wanaoapishwa leo.

  Marafiki wasomi wenzangu,
  Kazi ya uwakili ni kazi ngumu na inayohitaji umakini. Umakini unahitajika kwa kuwa mna wajibu wa aina mbili:

  Wajibu wa kwanza ni kwa mteja wako. Unapaswa kumlinda na kumtetea kwa kutumia ujuzi na maarifa ili kuhakikisha kuwa haki yake iliyopotea au iliyo katika hatari ya kupotea inalindwa.

  Wajibu wa pili ni ule ulionao kama afisa wa mahakama. Wajibu huu unakutaka umsaidie Jaji au Hakimu kutenda haki kulingana na sheria. Ni vizuri tukumbushane kuwa kuna mazingira ambapo wajibu huu naweza kuwa mkubwa zaidi kuliko ule ulionao kwa mteja wako, nao ni pale unapohitajika kutofanya chochote ambacho kitaipotosha Mahakama.

  Mheshimiwa Jaji Mkuu,
  Kabla sijahitimisha hotuba yangu ningeomba nitoe rai kwa mawakili wapya. Mnajiunga na fani ambayo inajisikia raha inapoitwa "a noble profession". Ni muhimu kwenu kuzingatia kwamba nobility si jambo la kurithi, na wala si jambo la kujipachika tu kwa kujiita hivyo. Nobility ni sifa ambayo ni lazima itokane na vitendo vyetu kama wanasheria na kama mawakili. Tuna wajibu wa kuhakikisha kwamba tunailinda heshima hiyo kwa vitendo vyetu, kwamba jamii (ya sasa na ya vizazi vijavyo) inatambua na itandelea kutambua hivyo. Jamii itafanya hivyo si kutokana na sisi wenyewe kujiita "a noble profession", bali kwa matendo yanayoendana na sifa hii adhimu.

  Mheshimiwa Jaji Mkuu,
  Naomba nihitimishe hotuba yangu kwa kutoa mwaliko kwa wanachama wetu, wapya na wa zamani. Mara nyingi tunapokuwa na sherehe kama hizi, huwa tunawaandalia mawakili wapya semina fupi, ambayo hufanyika siku hiyo hiyo ya sherehe. Kwa mwaka huu, kuna tofauti kidogo. Safari hii tutaifanya kesho kutwa, tarehe 17 Desemba, kuanzia saa 4:00 asubuhi katika ukumbi wa Ubungo Plaza na itakuwa inampatia wakili pointi nne (4) za CLE. Tafadhali msikose. Baraza la Uongozi la chama limeamua kuwa mawakili wote mnaosajiliwa leo mtahudhuria mafunzo haya ya siku nzima bila malipo yoyote. Karibuni Sana.

  Mheshimiwa JaJi Mkuu,
  Baada ya kusema hayo, naomba niwasilishe salamu za Chama Cha Mawakili Tanganyika katika hafla hii. Napenda pia kuwatakia nyote Krismasi njema na heri ya mwaka mpya.

  Asalaam Aleykum.

  Dr. Fauz Twaib
  14 Desemba 2009
   
Loading...