Tanganyika, jina la taifa la watu lilopotea

mwanakidagu

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
208
78
Tanganyika nchi ya watanganyika iliyopotea kisa muungano.Yupo mtanganyika mmoja kwa jina anaitwa CHRISTOPHER MTIKILA ameidai nchi yake takriban miaka 20 hv bila mafanikio.

Ipo siku watanganyika watapata uhuru wa taifa lao lililoporwa na muungano feki unao maliza kodi zetu kwa kuundwa kwa kamati za kunusuru muungano huu feki.
 
Tanganyika kama Palestina...ni nchi iliyopotea katika ramani ya dunia! Ukitaka kuiona Tanganyika soma vitabu vya historia!
 
Kwahiyo Tanganyika imo kwenye vitabu vya historia? Aibu!!!
 
Kwa hili sisi Watanganyika ni wajinga na wapuuzi kwa kuikumbatia CCM. Tulaaniwe
 
Jaji Warioba tutakukumbuka kwa jambo kubwa moja, kuirudisha nchi ya Tanganyika kupitia katiba mpya.
 
Jaji Warioba tutakukumbuka kwa jambo kubwa moja, kuirudisha nchi ya Tanganyika kupitia katiba mpya.
Mie nilimuomba aheshimu maamuzi ya tume mbili za majaji Nyalali na Kasanga kuhusu dawa ya muungano huu.
 
Tulieni vijana na wazee, mmeshindwa kutafutia uhuru wa taifa lenu kwa kuonesha vitendo. Lingekuwa swala la chadema na ccm mngeingia barabarani lakini hamjawa tayari kulipigania taifa. Tulieni tukutafutieni taifa lenu kwa vile mmeshindwa kulipigania, sisi wazanzibari tunapigania letu, tukifanikiwa basi na nyie lenu mtakua nalo tayari! :)
 
Fanyeni kazi mpate maisha mazuri. Huu upuuzi wa kulilia jina utawasaidia nini? Wakati mnahangaika kuitafuta Tanganyika, wenzetu wa akili finyu wameishia kwenye bodaboda. Huku nyuma ardhi inapokwa na wageni na watu weupe. Ninyi badala ya kuhanagikia uchumi, mnalilia "jina". Haya, na kesho iwe Tanganyika, watoto wetu ada zitapunguzwa shuleni? Watapata mlo sahihi? Watatibiwa kama anavyostahili binadamu kutibiwa? Mtapata maji kwenye mabomba? Acheni ujuha. Iwe Tanzania, iwe Tanganyika, bila kujibidisha kwa haki, na kupambana na hawa majizi wa mali za umma, ni kazi bure.

Nawasilisha

Manyerere
 
Back
Top Bottom