Tanganyika Government

Tanganyika Government

Kwanini umesema hivyo?
Kama tutakuwa na visiwa viwili nadhani ni Mafia na Unguja

kwa jinsi zoezi la katiba moya linavyoenda, inaonekana Wananchi wa Unguja hawapendi muungano na wapo tayari kwa lolote ili wajitenge. wenzao wanaotokea Pemba wanajua faida ya muungano cz wanafanya sana biashara huku bara. watu wa bara hawaoni kabisa faida ya huo muungano.

iwapo raia hao wakipewa uhuru wa kuchagua hatma yao, Unguja itajitenga. ila Pemba hawatakubali.

na wazee wenye nchi hawataki masuala ya serikali tatu.

Mwl. Nyerere alishaona hili tangu karne zilizopita. tatizo siku hizi wazungu wanakuja na masuala yao ya Human Rights kwa hiyo itatukaba hapo mbeleni kama tunang'ang'ania.
China waliachana na Taiwana ila jamaa wanataka kurudi sasa hivi.

Hong kong wenyewe wanatamani kujiunga na China
 
yafaa kwa waliolaza kalenda kama mimi na mzizi mkavu
 
Come sun come rain...hii tanganyika ni lazma irudi...mpaka kieleweke...

Haijalishi umekwenda umbali kiasi gani ila kama hauko katika njia sahihi ya kufika uendako..rudi nyuma anza upya safari yako ili ufike huko ulikokusudia kwenda

huu muungano haujatufikisha tunakotaka kwenda so ni bora kuuvunja na kuanza upya mwaka 1964...tutakuwa tumepoteza miaka 50 ya kujifunza kutokana na makosa yetu.
 
Back
Top Bottom