Kikwajuni One
JF-Expert Member
- Mar 18, 2013
- 13,149
- 6,989
Mwalimu wa shule ya secondary ya Mkwakwani,jijini Tanga,amempiga mwanafunzi wa kidato cha nne,Mohammed Seleman, wa shule hiyo mpaka kupooza.
Kutokana na kuchelewa shule,mwanafunzi huyo aliyepekekwa katika hospital ya mkoa wa Tanga ya Bombo,na kupewa uhamisho wa kwenda hospital ya Taifa ya Muhimbili,jijini Dar es salaam,amepooza kuanzia sehemu aliyopigwa,kuendea chini kwenye miguu.
======
Jeshi la Polisi mkoani Tanga linamshikilia mwalimu wa Shule ya Sekondari Mkwakwani kwa kumpiga na kumsababishia madhara ya kiafya mwanafunzi, Suleyman Mohamed (18).
Mwanafunzi huyo inadaiwa alichapwa viboko juzi asubuhi na mwalimu huyo wa zamu aliyekuwa akiwaadhibu wanafunzi waliochelewa na waliokuwa wakipiga kelele darasani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba amesema tayari mwalimu huyo yuko mikononi mwa jeshi hilo na upelelezi wa suala hilo unaendelea.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa amewataka walimu kuwa waangalifu wakati wakiwaadhibu wanafunzi ili kukwepa madhara kwa wanafunzi.
“Tunalifuatilia kwa karibu tukio hili. Niseme kwamba tutachukua hatua stahiki ikithibitika kuwa umefanyika uzembe,” amesema Mwilapwa.
Baada ya kuchwapwa, mwanafunzi huyo amelazwa katika Hospitali ya Rufani ya Bombo ikielezwa kwamba tayari amepatiwa rufaa kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.
Chanzo: Mwananchi