Tanga: Kange Kasera viwanja vya wananchi vinauzwa kwa jamaa wa maafisa ardhi na wafanyabishara kinyume na agizo la waziri

kisingi

JF-Expert Member
Apr 9, 2014
516
377
Kasera Kange Tanga kuna mgogoro mkubwa wa viwanja vya wanyonge na masikini kuuzwa kwa wafanyabiashara na jamaa wa maafisa ardhi Straton (Toni) na Mruma na si kurasimisha kama alivyo agiza Waziri Lukuvi katika mkutano na wananchi March, 2019. Waziri alitoa miezi sita hadi mwaka wanyonge masikini watafute pesa ndani ya muda huo warasimishiwe.

Kinyume na agizo hilo baada ya waziri kuondoka maafisa hawa wa ardhi na mkurugenzi wa jiji walitoa muda wa wiki moja hadi mwezi na taarifa haikutolewa kiuhalali kwa wananchi hivyo wengi wao kukwama. Kilichofuata ni vishoka kupita usiku na kuuza viwanja walivyo vipenda kwa idhini ya maafisa ardhi na hata beacon huwekwa usiku mashahidi ni wakazi wenyewe wa Kasera Kange.

Mkuu wa wilaya ameunda kamati ambayo inashindwa kumkabili Toni kwani aliyowauzia viwanja vya wanyonge wanaendelea kujenga tena kwa dharau kubwa. Kamati ni jambo la maana lakini haiwezi kuwakabili Toni na Mkurugenzi eti wanabaraka za msajili wà hazina kutafuta pesa kwa ajili ya manispaa ambayo ili feli kufikia lengo kimapato.

Wananchi zaidi ya sabini tayari wamefikisha malalamiko yao mbele ya kamati ya DC lakini ni watu wawili tu wamerejeshewa viwanja vyao mmoja akiwa ni mwanajeshi. Tunaomba serikali iingilie kati hili suala wananchi hawana imani na hawa vingozi waliotajwa hapa Tanga.
 
Huu wizi aliubariki Lukuvi, suluhisho ni Magufuli, basi! Haya mengine ni kujisumbua. Labda kujaribu kwa Bashiru, anaweza kwenda kwa Magufuli akamweleza.
 
Matatizo ya ardhi ni janga kubwa na tamaa ni mbaya sana kwani wanapowajibishwa sana sana ni kugukuzwa kazi au kubadilishwa makazi huku wakipeta na hela za kujipatia kwa njia mbaya.

Kama wanapatikana na makosa hayo wangefilisiwa tu.
 
Kwa manispaa ya Tanga maafisa ardhi wanafanya watakavyo kwa kuwa wako karibu na waziri wa ardhi na hata waziri alipo kuja Tanga alilishwa maneno na kinywaji kilimfanya kukoromea wakazi wa Kange kabla ya kutoa maelekezo ya kurasimisha viwanja ndani ya mwaka mmoja agizo ambalo Straton yaani Toni na Mruma wamelikaidi kwa kushirikiana na mkurugenzi wa mji wa Tanga kuamua kuuza tena viwanja na si kurasimisha.

Ninavyo andika ujumbe huu kuna dada mmoja rafiki wa Mruma anaitwa Presila ameuziwa kiwanja cha mtu na huyu Mruma amemuelekeza ajenge haraka ili pindi kamati itakapo pita kwenye kiwanja yeye aonekane amekifanyia kazi. Cha ajabu huyu Presila amevunja hata beacon na kufukia msingi wa awali wa mwenye kiwanja na kuchimba wa kwake.

Toni na Mruma wanasababisha matatizo makubwa ya ardhi hapa Tanga. Suala hili waziri Lukuvi hawezi kulitolea maamuzi kwa sababu hawa watu wawili wanasema wapo karibu nae hana ubavu wa kuwatumbua wanamjua A-Z.

Tunaomba rais kwa kutumia vyombo vyake alishughulikie suala la kuporwa viwanja wanyonge wa Kasera Kange Tanga na kuuzwa kwa mahawara na wafanya biashara wanao wapa mlungula maafisa ardhi.
 
Ni kweli kabisa yanayo zungumzwa kwenye kamati ya DC huyu Mruma anayajengea taswira ya kumlinda hawara yake Presila na amemwambia ajenge haraka katika kiwanja cha mzee wa watu aliyestaafu na yeye atamlinda kwa nguvu zote na kamati ni kiini macho tu kilicho tengenezwa na mkuu wa wilaya.
 
Nilisikiaga Tanga kwa uchawi mko juu. Si mumpige kipapai huyo Mruma awe mkojo unatokea sehemu ya haja kubwa.
 
Hawa maafisa wa ardhi wako juu kwa uchawi kwa sababu wanajua wanaowadhulumu wengi ni wanyonge na wazee. Toni na Mruma wana waganga wao Handeni zigua na upare ndio maana wako jeuri na juu ya waziri wa ardhi ambaye ni kama ana waogopa.
 
Pole sana Mr Kisingi
Nimejaribu kusoma andiko lako hili kama Mtanzania mwenzio nimegundua huenda unatatizo la kisaikolojia linalokusumbua.Serikali yetu hii pendwa haiendeshwi kwa majungu kama uliyoyaleta hapa Jamiiforums.

1. Kange kasera hakuna zoezi la urasimishaji lililofanyika, naona kwenye andiko lako umemlisha maneno Mh waziri na kumtuhumu pia.Eneo lile ni shamba is serikali ambako lilivamiwa.Vishoka walianza kuunza maeneo hayo kwa watu mbalimbali na licha ya jitihada za serikali kueleza wananchi wasinunue maana uuzwaji sio halali bado wapo ambao waliwaamini vishoka kuliko serikali.Mimi binafsi nakiri kuuziwa na kishoka bila kujua.Nilikuwa kuelewa baadae.

2. Katika baadhi ya vishoka walikuwa wamejimegea viwanja zaidi ya 300 mtu mmoja.Yaani mtu mmoja anamiliki viwanja 300 na zaidi yeye mwenyewe.Mh waziri akaja na suluhisho kwamba Kwa kuwa wapo waTz wengi maskini wanyonge tayari wameingizwa chaka basi wanunue viwanja hivyo kwa bei ya 1500/= kwa sqm moja..Na hii yote ni huruma ya Waziri kwa sababu kiuhalali viwanja vile mauziano ambayo wananchi waliyafanya na vishoka hayatambuliwi na serikali.Kiuhalisia bei halisi ya kuuza viwanja kange kasera haitakiwi kuwa chini ya 15,000 kwa sqm moja.

3. Sasa mr kisingi mbona mimi mwananchi mwenzio japo nilikuwa na msingi tu nimeruhusiwa kulipia kidogo kidogo mpaka mwaka kama alivyoagiza Waziri.Nawaonea sana huruma hao maafisa maana sisi wananchi wengi hatuna fadhila.Viwanja cha milinga zaidi ya 300ambaye ndo kishoka aliyetuliza wengi vilitangazwa kwa wananchi wote anayetaka kununua akanunue.Muda mwingine tusiwe na mihemko tukakosa huruma lakini tuweke siasa kando na kusikiliza maelekezo ya serikali.

Siku ya ujio wa waziri lukuvi diwani wetu alitulisha maneno tukaamini kama ule ni urasimishaji na tunatakiwa kulipa 250,000 tu.Lakini Mbona Mh waziri alieleweka vzr?
 
Changu ilibidi nikilipie tena kwa mara ya pili
Mara ya kwanza ulikilipia kwa nani ?? Mimi nililipa kwa mwenyekiti Mzee rajabu Sasa hapo ni kuhesabu kama umelipia mara ya pili ?Kama kweli tumelipa serikalini mara mbili tunahaki ya kulalama lakini wengi tuliwalipa vishoka.Tuwe wa kweli.
 
Marias hii habari yako umeitunga kwa sababu sio sawa na siyo hali halisi Hii inathibitisha kuwa wewe ni mmoja wa wanufaika na mpango wa idara ya ardhi Tanga ya kuuza viwanja vya watu ama wewe ni kishoka wa ardhi Tanga mliodanganya kuwa kuna mtu ana viwanja zaidi ya 350 na kuanza kupora viwanja vya watu na kuviuza tena kwa mahawara wa wafanyakazi wa mipango miji na wafanya biashara. Tunawajua vishoka wote kwa majini mnao shirikiana na Toni na Mruma na wengine.

Kama hakuna tatizo mbona wananchi zaidi ya 70 wamekwisha fika mbele ya kamati ya DC na kutoa malalamiko yao na wapo wengine hawakuwahi kwa kuwa muda wa kamati haukutosha na kila siku kulikuwa na ambao wamekosa nafasi ya kuhojiwa.. Ninyi vishoka ndiyo mliopeleka uwongo kuwa Millinga ana viwanja 350 ili mpewe tenda ya kuonyesha viwanja vya watu na viuzwapo mnapata chochote kitu. Kazi hii mnaifanya usiku na wakazi wa Kasera wanalijua hili na DC alishaelezwa katika mkutano. Hadi sasa kati ya hao watu walio lalamika mbele ya tume ni wawili tu walio uziwa na milinga kitu ambacho si cha ajabu wala kosa.

Hii ina bainisha kuwa ninyi vishoka mmechangia sana viwanja vya watu kuuzwa tena badala ya kurasimisha. Nenda Kasera masai kaone ushahidi Presila alivyo uziwa kwanja cha mtu na sasa amefukia msingi uliyokuwepo na yeye kuanza ujenzi haraka akisaidiwa na Mruma. Ametengenezewa kiwanja kwa kupora sehemu ya kiwanja cha mtumishi wa kiroho na cha mzee mmoja mstaafu.

Wewe naona unajibu kutetea watumishi wa ardhi kwa kuwa ndio mnao umiza wananchi wa hali ya chini na mengi uliyo andika sio uhalisia. Kama utaendelea kuleta uwongo nitaleta list ya vishoka na hata viongozi wa Tanga waliojimilikisha viwanja Kange.
 
Kuhusu waziri ninacho sema yeye ametoa hadi mwaka kurasimisha lakini viongozi wa jiji na mipango mji Tanga kwa maana ya idara ya ardhi wamekaidi agizo la waziri na kutoa wiki moja hadi mwezi mmoja hii ili kuwa March,2019. Agizo la waziri linge koma March, 2020. Baada ya hiyo March, 2019 ndiyo wakaanza kuuza viwanja vya wanyonge. Narudia waziri ametoa hadi mwaka kurasimisha, halimashauri na idara ya mipango miji Tanga wamekaidi wao wanauza viwanja vya wanyonge badala ya kurasimisha ushahidi ni wingi wa watu waliopeleka malalamiko kwenye kamati iliyo undwa na DC.
 
Endelea na mawazo yako mgando. Kama unaushahidi ulete hapa acha kutembelea kauli za mahawara. Tena usivyokuwa na akili timamu unataja hadi wake za watu na kuwadhalilisha. Kama unaushahidi wa unayoongea tuletee hapa hizo picha za kuthibitisha uhawara. Acha porojo
 
Kuhusu waziri ninacho sema yeye ametoa hadi mwaka kurasimisha lakini viongozi wa jiji na mipango mji Tanga kwa maana ya idara ya ardhi wamekaidi agizo la waziri na kutoa wiki moja hadi mwezi mmoja hii ili kuwa March,2019. Agizo la waziri linge koma March, 2020. Baada ya hiyo March, 2019 ndiyo wakaanza kuuza viwanja vya wanyonge. Narudia waziri ametoa hadi mwaka kurasimisha, halimashauri na idara ya mipango miji Tanga wamekaidi wao wanauza viwanja vya wanyonge badala ya kurasimisha ushahidi ni wingi wa watu waliopeleka malalamiko kwenye kamati iliyo undwa na DC.
Nini maana ya kurasimisha? Tatizo lako unajifanya unajua wakati haujui.Kubali kuelekezwa.
 
Naona povu lina kutoka kwa sababu wewe ni muhusika. Acheni kuuza viwanja vya wanyonge.
 
Back
Top Bottom