Wyatt Mathewson
JF-Expert Member
- Dec 22, 2017
- 10,182
- 24,684
Serikali imeombwa kubeba deni la shilingi trilioni 1.39 ambalo Shirika la Umeme nchini(Tanesco), linadaiwa na taasisi mbalimbali ikiwamo watoa huduma wake na mabenki. Katika deni hilo, shilingi bilioni 950, zinadaiwa na watoa huduma ikiwamo kampuni ya IPTL, Songas Pan Africa na TPDC, huku shilingi bilioni 442, zikiwa ni za mkopo wa benki kwa matumizi mbalimbali.
Mkurugenzi wa Tanesco, Dk.Tito Mwinuka, amesema shilingi bilioni 408 zilizokopwa kutoka benki zilitumika kununulia mafuta mazito ya kuendesha mitambo ya kufua umeme, na shilingi bilioni 34 zilitumika kulipa fidia ya ujenzi wa ilani kutoka Somangafungo hadi Kinyerezi.#KwanzaHabari
Reality strikes!
These motherfuckers are coming outta woodworks now!