Hahaha hiini tatizo
nafkiri mawazo yako ni ya msingi sana kama serikali wangekuwa wanapita kwenye majukwaa kama haya wangepata pa kuanzia big up!Mkuu, hoja yako ina mashiko ila, Tunahitaji wataalamu wa nje/ independent hydrologist kuchunguza flow mita za kabla maji kuingia Mtera, levels at dam, bypass, flow downstream before Kidatu na correlation ya before Kidatu na downsteam, Hili litaondoa kiwingu na kuipa haki TANESCO. Pia weKeni CCTV cameras kumonitor water gates. Mashamba ya mpunga mengi upstream yamedoda, uzalushaji mdogo na bado umeme tabu.
Tanesco yacharuka! Hamishahamisha yaanza
Habari za uhakika tulizozipata kutoka kwa mdau wa ndani ya shirika la umeme nchini TANESCO zinasema kwamba pamekuwa na mtikisiko mkubwa wa mameneja na maofisa waandamizwi kuhamishwa vituo, zoezi linalosemekana lina nia ya kuboresha huduma na kuimarisha ufanisi.
Kwa mujibu wa chanzo hicho cha habari miongoni mwa maofisa wanaohamishwa ni pamoja na mameneja wa mikoa ya morogoro na arusha waliokuwa wanalalamikiwa kwa matatizo ya mita katika mikoa hiyo.
Wengine ni mameneja wa mikoa ya Manyara, Lindi, Tabora na Temeke.
Pia inasemekana shirika hilo limeunda tume ya kuchunguza tuhuma za kufunguliwa maji katika bwawa la Mtera. Pia chanzo chetu kinaonyesha kwamba wakuu wote wa vituo vya kuzalisha umeme wamehamishwa vituo.
daah, nikadhani wamecharuka na kuanza kuzalisha umeme kwa ufanisi bila upuuzi wao wa kukata-kata umeme hovyo bila maelezo
wanazalisha nini?tanesco hawazalish umeme
Ngoja kwanza niende mahali faragha nilieeee kasha nitarudi kuchangia kwani nina hasira sana bila kulia nitatukana!
Kwanza huyo meneja Wa ARUSHA mwezi Wa 3 Leo naendaga hapo .naambiwa amesafiri Mara yuko site Mara Yuki dar.yaani kwa ujumla ni ajafika ofisini mwezi Wa 3 Leo.yaani badala ya kutimuliwa wanahamishwa...kwa hiyo wanahamisha matatizo toka Morogoro na Arusha kwenda sehemu zingine