Tanesco yacharuka! Hamishahamisha yaanza
Habari za uhakika tulizozipata kutoka kwa mdau wa ndani ya shirika la umeme nchini TANESCO zinasema kwamba pamekuwa na mtikisiko mkubwa wa mameneja na maofisa waandamizwi kuhamishwa vituo, zoezi linalosemekana lina nia ya kuboresha huduma na kuimarisha ufanisi.
Kwa mujibu wa chanzo hicho cha habari miongoni mwa maofisa wanaohamishwa ni pamoja na mameneja wa mikoa ya morogoro na arusha waliokuwa wanalalamikiwa kwa matatizo ya mita katika mikoa hiyo.
Wengine ni mameneja wa mikoa ya Manyara, Lindi, Tabora na Temeke.
Pia inasemekana shirika hilo limeunda tume ya kuchunguza tuhuma za kufunguliwa maji katika bwawa la Mtera. Pia chanzo chetu kinaonyesha kwamba wakuu wote wa vituo vya kuzalisha umeme wamehamishwa vituo.