IZENGOB
JF-Expert Member
- Jun 28, 2014
- 323
- 317
Nikiwa mmoja wa waathirika katika sakata hilo leo nimeyastaajabu ya Mussa pale nilipoenda Tanesco kuulizia kuhusu mita yangu kukataa kununua umeme,nikiwe ndani ya ofisi hizo nilishikwa na butwaa baada ya kuambiwa kuwa watumiaji wa umeme wadogo (TARIF 4) ambao walikuwa wakinunua umeme wa 9,050 wanapata UNIT 72 wapo kwenye mchakato wa kufutwa na kupelekwa Tarif 1, Ambapo watumiaji hawa wakinunua umeme wa Tsh. 10,000/= wanapata UNIT 28.
Kilichonishangaza zaidi ni usiri wa jambo hili ambalo linalenga kuwaumiza watanzania wa hali ya chini.Nilipouliza zaidi kuhusu hilo nielezwa kuwa hata kama unatumia taa moja utapelekwa kwenye TARRIF 1 ambayo kwa mujibu wa maelezo ya Katibu mkuu Wizara ya nishati na madini alisema kuwa Tariff 1 ni umeme wa majumbani walio na matumizi makubwa(viwanda vidogo).
Nasikitika waziri mwenye dhamana ambaye alionekana kuwatetea wananchi wa hali ya chini wanaotumia umeme chini ya Unit 70 kwa mwezi yupo kimya,Pia Mtukufu alionekana kuzungumzia suala hilo kanisani akidai kuwa yeye ni mtetezi wa watanzania wa hali ya chini.
Kwa mantiki hiyo nathubutu kusema kuwa TANESCO WAMEPANDISHA GHARAMA ZA UMEME KIAINA.