Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,408
- 13,259
Kwenye taarifa ya habari ya ITV tarehe 11/03/2016 niliona wakati EWURA wakijadili ombi la TANESCO kutaka kushusha bei ya umeme wakisema wadeni wakubwa wa TANESCO ni pamoja na Zanzibar inayodaiwa zaidi ya Shilingi bilioni 106, serikali (nadhani walimaanisha Tanganyika) wanaidai bilioni 33 na watu binafsi bilioni kadhaa.
Hapo ndipo niliposhangaa kuwa kwa deni lote hilo kwanini TANESCO hawaikatii umeme Zanzibar kama wanavyokata kwa watu binafsi wanaodaiwa sana sana elfu au laki kadhaa.
Vile vile nikashangaa kuwa baada ya kupindua uchaguzi wa wananchi katika uchaguzi wa Decemba mwaka jana wanaitisha uchaguzi mwingine utakogharimu zaidi ya bil 4 wakati tayari wameshasema liwake jua au mvua inyeshe lazima wao watawale kwanini wasingetumia hizo pesa kupunguza deni la TANESCO?