maroon7
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 11,345
- 15,852
Wakuu hii shida wanaotupatia tanesco kwa kutufungia mita za kwenye nguzo ambazo zinakata umeme kisa eti Low voltage ni hujuma. Nasema hivi kwa sababu wao wanalitambua tatizo hili na mbaya zaidi wanasema hizo mita hazina ufumbuzi labda itokee tatizo liishe lenyewe. Hii inasikitisha sana kila siku umeme kukatika na kurudi baada ya masaa kadhaa na hata baada ya siku kadhaa kupita. Naomba hawa watu watumbuliwe kwa uzembe wanaoukumbatia na kutuhamishia wananchi matatizo wakati tayari tunayo ya kutosha.