TANESCO wameweka nguzo katikati ya kiwanja changu

TANESCO wameweka nguzo katikati ya kiwanja changu

Ardhi Ni Mali Ya Serikali, Tunakodishwa Tu Kwa Pesa, Ile Hati Ya Kiwanja Ndo Maana Ina Muda Kabisa Unachofanya Ni Kurenew. Ss Km Kila Mtu Hatataka Nguzo Ktk Kiwanja Chake TANESCO Waweke Wapi? Hyo Co Kesi, Umeme Ni Maendeleo Ambayo Hata Ww Hyo Nguzo Utaitumia Wkt Unataka Kuweka Huo Umeme. Cha Kufanya Nenda Kawaeleze Kuwa Pale Walipo Weka Unataka Upatumie Na Hvyo Waje Ili Muone Mahala Pazuri Pa Kucmika Nguzo. Ila Km Utapata Usumbufu Wwte Muone Meneja Wa Kanda Yenu, Akikuzingua Mwambie Utaenda Makao Makuu Kwa Mabosi Wake, I Hope Hawawez Kukuzngua, Hz Ni Zama Nyingine Aisee.
 
Salaam wana JF.

Katika hangaika zangu za hapa na pale, nilisafiri mbali na mkoani kwangu na nilikaa kwa miaka kadhaa. Baada ya kurudi, nakuta kuna nguzo ya umeme imesimikwa katikati ya kiwanja changu ilihali nilitaka kupajenga. Kilichotokea ni kwamba, kuna jirani alivuta umeme na wakapitisha juu ya kiwanja changu jambo linalopelekea kiwanja changu kuwa kidogo kwa kujenga. Pia hata nikisogea upande mmoja, kamba zitakuwa juu ya paa la nyumba. Naombeni ushauri wa nini chakufanya na taratibu zipi nichukue katika kutatua hilo tatizo.
Walifanya hivyo hivyo kwenye kiwanaja changu. Nilikuwa sijatokea kama miezi 8 Tanesco wakaja kumuunganishia jirani umeme wakaweka nguzo katikati ya kiwanja changu. Nilipokuja kujenga niliwapigia simu wakaja kuhamisha hio nguzo. Sasa hivi iko pembeni.
 
Siyo kweli hata kidogo, mtaani kwetu tuna watu wenye shida hiyo tangu 2010 hadi dakika hii wamenyosha mikono, wamefuatilia Tanesco mpaka ikaonekana kama vile wanafuatilia ajira, wametoa taarifa makao makuu nako ni yaleyale!!

ndiyo maana tunashauri iwepo namba ya simu ya boss wao wizarani awe anawaamuru kwenda kufanya kazi hizo, lakini kama utategemea Regional Managers umekula wa chuya
Kwangu waliihamisha ndani ya wiki tu. Kazi kama itahitajika nguzo ingine, ila kuhamisha sio issue.
 
Mkuu nenda tu tanesco ukaeleze tatizo lako hiyo nguzo itahamishwa bila tatizo lolote
.....Kusema itahamishwa bila tatizo si kweli, lazima wamtoe pesa hapo.
 
Nenda tanesco ,inawezekana jirani yako aliwadanganya tanesco kwa kuwambia ni eneo lake ilitakiwa wakujulishe ili uje uwaelekeze sehemu ya kuweka hiyo nguzo sababu hata wewe utahitaji umeme baada ya kujenga hiyo nyumba yako
 
Inazungumzika hiyo,kawaone! Usiende mikono tupu tafadhali tafadhali
 
Mahakamani kesi itachukua miaka 3 ,na utashangaa mnaibua mambo mengine, usikute huna hati, hujalipia kiwanja, mipango miji n.k

Mlipe mvuta bangi akaikate na shoka anasepa anabeba na kipande cha nguzo itaonekana kachukua sababu ya kuni, kumbe lengo limetimia
Hahahahah mmhh nimejikuta nacheka kwa huu ushauri wako...
Wewe ulishawahi kufanya hivyo
 
Back
Top Bottom