TANESCO wameweka nguzo katikati ya kiwanja changu

JMF

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
1,751
2,749
Salaam wana JF.

Katika hangaika zangu za hapa na pale, nilisafiri mbali na mkoani kwangu na nilikaa kwa miaka kadhaa. Baada ya kurudi, nakuta kuna nguzo ya umeme imesimikwa katikati ya kiwanja changu ilihali nilitaka kupajenga.

Kilichotokea ni kwamba, kuna jirani alivuta umeme na wakapitisha juu ya kiwanja changu jambo linalopelekea kiwanja changu kuwa kidogo kwa kujenga. Pia hata nikisogea upande mmoja, kamba zitakuwa juu ya paa la nyumba.

Naombeni ushauri wa nini cha kufanya na taratibu zipi nichukue katika kutatua hilo tatizo.
 
Fanya mipango huitoe hiyo nguzo hapo mbele ya safari hawakawii kusema hata kiwanja ni cha kwao wao
 
Ikate tu hiyo nguzo hapo (Ingekuwa mimi lakini)

Njoo usiku ikate na shoka ianguke kabisa au chain saw bila hujuma utadhulumiwa
 
Peleka taarifa tanesco kwa maandishi ikiwa na Reference pia weka muda wako maalum wawe Washaondoka katika eneo.
Hatua ya pili ikiwa wanashindwa kuondoa hio nguzo, Peleka Case mahakamani, uhakika utashinda na gharama hata fidia watalipa.

Kama unataka njia ya mkatato tafuta shoka ikate hio nguzo just kidding
 
Inaboa kweli yaani mimi nilikuta wameiweka ndani ya kiwanja ila kwa pembeni, wakati ukuta unajengwa imekaa kwa ndani.
 
Hao wanaokushauri uikate sijui na shoka au ufanye ubabe wanakosea sana.....
Fuata taratibu nenda tanesco ukiona Hanna maelewano nenda mahakamani mbona kitaeleweka tuu
 
Salaam wana JF.

Katika hangaika zangu za hapa na pale, nilisafiri mbali na mkoani kwangu na nilikaa kwa miaka kadhaa. Baada ya kurudi, nakuta kuna nguzo ya umeme imesimikwa katikati ya kiwanja changu ilihali nilitaka kupajenga. Kilichotokea ni kwamba, kuna jirani alivuta umeme na wakapitisha juu ya kiwanja changu jambo linalopelekea kiwanja changu kuwa kidogo kwa kujenga. Pia hata nikisogea upande mmoja, kamba zitakuwa juu ya paa la nyumba. Naombeni ushauri wa nini chakufanya na taratibu zipi nichukue katika kutatua hilo tatizo.
Mijirani mipumbavu ya hivyo imejaa tele. Kuna mmoja alitaka kupitisha barabar kwenye kiwanja changu, nilichomfanya mpaka leo hawezi kunitazama usoni.
 
Salaam wana JF.

Katika hangaika zangu za hapa na pale, nilisafiri mbali na mkoani kwangu na nilikaa kwa miaka kadhaa. Baada ya kurudi, nakuta kuna nguzo ya umeme imesimikwa katikati ya kiwanja changu ilihali nilitaka kupajenga. Kilichotokea ni kwamba, kuna jirani alivuta umeme na wakapitisha juu ya kiwanja changu jambo linalopelekea kiwanja changu kuwa kidogo kwa kujenga. Pia hata nikisogea upande mmoja, kamba zitakuwa juu ya paa la nyumba. Naombeni ushauri wa nini chakufanya na taratibu zipi nichukue katika kutatua hilo tatizo.
Upo mkoa gani
 
Hao wanaokushauri uikate sijui na shoka au ufanye ubabe wanakosea sana.....
Fuata taratibu nenda tanesco ukiona Hanna maelewano nenda mahakamani mbona kitaeleweka tuu

Mahakamani kesi itachukua miaka 3 ,na utashangaa mnaibua mambo mengine, usikute huna hati, hujalipia kiwanja, mipango miji n.k

Mlipe mvuta bangi akaikate na shoka anasepa anabeba na kipande cha nguzo itaonekana kachukua sababu ya kuni, kumbe lengo limetimia
 
Mkuu kwanza hicho kiwanja kimepimwa na kina hati..? Kama jibu ni ndio Tanesco watakuwa wamevamia kiwanja chako.. So sheria itakuwa upande wako na unachotakiwa ufanye ni uende na hati zako Tanesco.. Watahamisha mara moja..

Kama kiwanja chako hakijapimwa lakini kina hati ya makazi pia unaweza kufuata utaratibu huo huo wa kwenda Tanesco na hiyo hati ya makazi, mtasikilizana na mwisho wataziondoa..

Kama kiwanja chako hakijapimwa na wala hakina hati ya makazi, then itabidi uende kwenye idara ya mipango ili uangalie eneo hilo la kiwanja chako limetengwa kwa shughuli gani..
 
Tanesco hawana shida. Wao waliambiwa kuwa hicho kiwanja ni Mali ya jirani. Wangeambiwa ukweli wasingesimika Nguzo hiyo.

Nenda uwaambie ukweli wataitoa tu. In waungwana sana siku hizi.
 
Mkuu nenda tu tanesco ukaeleze tatizo lako hiyo nguzo itahamishwa bila tatizo lolote

Siyo kweli hata kidogo, mtaani kwetu tuna watu wenye shida hiyo tangu 2010 hadi dakika hii wamenyosha mikono, wamefuatilia Tanesco mpaka ikaonekana kama vile wanafuatilia ajira, wametoa taarifa makao makuu nako ni yaleyale!!

ndiyo maana tunashauri iwepo namba ya simu ya boss wao wizarani awe anawaamuru kwenda kufanya kazi hizo, lakini kama utategemea Regional Managers umekula wa chuya
 
Back
Top Bottom