TANESCO tuoneeni huruma na hili joto

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,767
29,721
Wadau,

Hivi karibuni mamlaka ya hali ya hewa ilitangaza kuongezeka kwa joto kutokana na Jua kusogea karibu zaidi kutokana na kua juu ya Ikweta. Sasa basi tangazo au habari hizi niwazi sote tulizisikia wakiwemo watendaji wa TANESCO.

Ukweli muda kama huu wa mchana majumbani ni AC na mafeni mtindo mmoja lasivyo mtu unaungua bila kujijua. Hatuna uwezo wa Solar wala Jenereta na wala sio wote tuliobahatika kujenga maeneo ya ufukwe au milimani kwenye upepeo wa asili. Hiki ndicho kile kipindi ambacho wangekua na huruma tu na sisi tukaendelea kuwalipa hizo charges zao kwa kuwahsa feni 24/7.

Kutukatia umeme kipindi hiki cha joto ni kutukatili na kutuchumia dhambi za bure maana tunajikuta tunatoa maneno ya hasira either kimoyomoyo au kwa wazi kwa TANESCO. Tunaomba tusichumiane dhambi enyi TANESCO, kuweni na huruma na sisi wanachi. Ingekua hata tuko kipindi cha baridi tungeona poa tu, lakini sio kwa sasa jamani.

Kutoka Jasho jingi inaweza kua ni nzuri ki afya kwa mwili kutoa uchafu lakini sasa jasho tunalolitoa huku tunaungua ngozi na tumekunja uso kwa hasira sidhani kama lina afya na faida peke yake bila madhara. Kwanza Jasho linalotoka kuanzia asubuhi hadi TANESCO wakirudisha umeme jioni ni jingi sana hivyo litakua lina hasara tu.

Chondechonde wahusika wa TANESCO pamoja na Waziri + Rais, tuoneeni huruma sisi wancnhi wa kipato cha chini tusioweza kumudu Solar au jenereta za kusukuma Mafeni au AC.
 
Pole sana kwa usumbufu na adha munayaoipata lakini ni wazi kuwa hakuna mgao wa umeme. Ila ukiina Umeme umekatika au ukatwa basi kuna itilafu au matengenezo yanaendelea na ndo maana kumekuwa na taarifa za Mara kwa Mara pindi Umeme unapo katika au unatarajia kukatika
 
Ndugu Shark na wateja wote wa Tanesco tunawapa pole kwa adha tunayoipata.kwanza kabisa Tanesco hamna mgawo wa umeme na haijawahi kutangaza kama kuna mgawo ni hitilafu ambazo zinatokea katika miundombinu ya Tanesco, ambapo kukifanyika ukarabati inabidi sehemu husika kukatwe umeme.Na ukarabati huu unaofanyika mara kwa mara una lengo la kuboresha hali ya upatikanaji umeme wa uhakika.
 
Je hayo matengenezo yanafanyika mpaka usiku? Maana TEGETA wengine inabidi kutoka nje tuliwe na mbu asubuhi wanarudisha halafu saa nne asubuhi tena wanakat da
 
Ndugu Shark na wateja wote wa Tanesco tunawapa pole kwa adha tunayoipata.kwanza kabisa Tanesco hamna mgawo wa umeme na haijawahi kutangaza kama kuna mgawo ni hitilafu ambazo zinatokea katika miundombinu ya Tanesco, ambapo kukifanyika ukarabati inabidi sehemu husika kukatwe umeme.Na ukarabati huu unaofanyika mara kwa mara una lengo la kuboresha hali ya upatikanaji umeme wa uhakika.
Uboreshaji gani jana mwenge mmekata saa4 mkarudisha sijui saa 5 ile yaani tunalala milango waz madirisha waz kuweni na utu jamani
 
Ndugu Shark na wateja wote wa Tanesco tunawapa pole kwa adha tunayoipata.kwanza kabisa Tanesco hamna mgawo wa umeme na haijawahi kutangaza kama kuna mgawo ni hitilafu ambazo zinatokea katika miundombinu ya Tanesco, ambapo kukifanyika ukarabati inabidi sehemu husika kukatwe umeme.Na ukarabati huu unaofanyika mara kwa mara una lengo la kuboresha hali ya upatikanaji umeme wa uhakika.
Sikatai kama kuna kitu kinaitwa hitilafu. But imekua frequently sana, na hata wakikata wanachelewa sana kuurudisha. Ni kama vile wanajivuta sana kuelekea eneo la tukio.
 
Back
Top Bottom