TANESCO: Tumepunguza makali ya upungufu wa umeme, wiki iliyopita ilikuwa Megawati 200-250, wiki hii 100-150

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,956
12,256
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeeleza kufanikiwa kupunguza makali ya upungufu wa umeme kutoka wastani wa kati ya Megawati 200 hadi 250 wiki iliyopita hadi wastani wa kati ya Megawati 100 - 150 wiki hii.

Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Maharage Chande amesema wameendelea kuchukua hatua mbalimbali kukabiliana na changamoto ya mgao wa umeme.

Akielezea jitihada za muda mfupi zilizokamilika tayari wameshakamilisha matengenezo ya mtambo mmoja wa kituo cha Kinyerezi namba II na umeshaanza kuzalisha megawati 45 za umeme kwenye Gridi ya Taifa kuanzia tarehe 24 Novemba 2022.

Pia amesema wamekamilisha matengenezo ya mtambo miwili iliyopo katika kituo cha Ubungo namba III na imeshaanza kuzalisha kati ya megawati 35 na 40 za umeme kwenye Gridi ya Taifa kuanzia tarehe 25 Novemba 2022.

 
Haya bhana

Ila kwetu huku......hali ni nafuu na kabla hizo megawatt hazijaingizwa kwenye grid ya Taifa

La muhimu wazipate hizo zilizosalia ili hawa wakataji wakose kisingizio
 
Stori za tarehe 25/11 na mgao upo pale pale zinatusaidiaje sisi?
 
Siku tatu zilizopita mvua ilinyesha Bukoba, radi ikaharibu transformer mbili maeneo jirani. Eneo moja ndio kwa naibu Waziri wa Nishati/Tanesco na eneo jingine wapo wakazi wa kawaida. Ajabu ndani ya saa moja baada ya mvua kukata eneo la Waziri lilikuwa limerudishiwa umeme na eneo la walalahoi bado mpaka leo hawajarudishiwa umeme.
Hii sio sawa Tanesco. Sikukuu ya Christmas sio sikukuu ya mateso
 
Ndio inavyokuaga
 
Ukute hamnunui Umeme

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…