TANESCO, tangazeni rasmi kuwa mgao wa umeme umeanza

Bongo ni zaidi ya uijuavy
SINA IMANI NA UKAWA
Ukawa ni hatari, Serikali ya Magamba Wamejinyenyea baada ya kusikia kuwa Ukawa Watakuwa Na Mkutano wa ki Historia Mwanza,Na Kuamuru TANESCO Kuhahakikisha watu hawafuatilii kinachoendelea Mkutanoni kwa Kukata Umeme Maeneo Mbalimbali ya Nchi,
Shame on You!!!
 
Tumieni Generator, na mtengeneze CD sijui DVD za kutosha ziendelee kuhubii kwenye migawahwa, kwenye mahoteli, kwenye vinyozi, vijiwe, magarini, kwenye mabusi tena mgawe bure kila busi lenye Screen ndani. Siku nyingine muwaombe ITV warushe muda watu wamekusanyika majumbani!.

Mwaka huu ccm wanalo.

Wanadhani kukata umeme ndiyo kuwanyima watu taarifa?

Ccm chini!, chini chini hadi kaburini!.

Ccm wanazikwa rasmi mwaka huu
 
TV zoteziko hewani nyie vipi acheni kupotosha sasa ni saa 9 Alasiri na Tv zote Star Tv na ITV kuna Filamu! Tupeni story nyingine!

Tatizo ni tv za watazamaji maeneo ya mbali na mkutano umeme majumbani mwao hakuna Tanesco wamekata, sasa hapo wataonaje? Yaani ni sawa na simu kama haina chaji sio kwamba mtandao haupo, mtandao unakuwapo ila simu ndiyo haina chaji. Tv zote sawa ziko hewani, lakini tv za majumbani mwa watu hazionyeshi sababu umeme umekatwa.
 
Kuna matangazo yalipita juzi Star tv katizo la umeme hata juzi na jana kwa baadhi ya maeneo ya Dar hakukua na umeme kutokana na marekebisho ya mitambo, au mnafikiri mitambo ya Tanesco inajua siasa?? Msizingue nyie kuingilia mambo yasiyowahusu!

Naona leo tanesco wamepata msemaji
 
Wakuu,baada ya CHADEMA kutangaza kufanya mkutano wa kihistoria jijini Mwanza leo tarehe 22/07/2015 saa 8 mchana.TANESCO wamekata umeme kanda ya ziwa tangu asubuhi mpaka sasa hivi.Je,hiyo ndiyo dawa ya CCM kuua upinzani kanda ya ziwa?

Wanazidi kumchezea sharubu simba
 
Hawa inaelekea hawajalipia airtime maana matangazo ya Tv huwa hayakatwi masaa 24 hata kama umeme haupo! tv z seeote sasa hivi hazina live coverage ya CDM kuna Filamu ndo zinaonyeshwa!sasa ni saa 9 walituambia kuanzia saa8 watakua hewani na sasa hawaonekani labda tusubiri watakuja saa 12!!

Mimi nina umeme wa jua (solar power) ni kweli hadi saa 9 mchana walikuwa hawajaanza kurusha matangazo ya mkutano live toka Mwanza, lakini right now mkutano uko hewani ITV live na hakuna umeme wa TANESCO tangu around saa 5asb huku Shinyanga!!

Tukubaliane na ewadau kwamba, hizi zinaweza kuwa ni hujuma 100% zenye lengo la kuzuia publicity dhidi ya upinzani hususani Chadema!!

Na huu kwa vyovyote ni ujinga na uwendawazimu uliovuka mipaka wa watawala wetu.

Just imagine wanaumiza na kutia hasara za mapato watu wangapi wakiwemo wana CCM wenyewe na wasio na vyama kwa kukata umeme masaa yote haya bila sababu zozote za msingi eti tu kwa kuihofia CHADEMA??

Tunasema bila sababu za msingi kwa sbb km kungekuwa na ishu ya kiufundi, wangetaarifu wateja mapema na tukajiandaa, lakini kwa hili hakuna anayeweza kuamini kuwa this is accidental technical fault iliyotokea by coincidence siku ambao upinzani wanafanya mkutano ambao wao wameuita wa kihistoria eneo ambalo mgombea wa CCM anatokea!

Na hili ndilo tatizo la kuchanganya siasa na shughuli za maendeleo ya watu........milele umaskini utaendelea kuwa dini yetu wabongo!!
 
wang'oe na nguzo kabisaa ili wasipate taarifa milele wananchi km ndio dawa
 
Back
Top Bottom