Tanesco tanesco tanesco tanesco

KIBURUDISHO

JF-Expert Member
Mar 28, 2011
1,002
274
Hivi Tanesco kwa nini mnafanya vitu ambavyo ukivifikilia kupitia kwenye kichwa chenye akili timamu unatamani ukamate kiboko uanze kuutandika uongozi mzima uliokaa ukasaini mikataba hii.Hivi kwa nini mnakubaliana na hao watu wanaowakodishia mitambo ya kuzalisha umeme kulipwa kwa siku kama ilivyokuwa kwa Richmond.? Kwa nini hawa wazalishaji wa umeme wasiwe wanalipwa kwa MEGAWAT wanazozalisha? Kama mwezi huu ataingiza megawat 100 alipwe hizo megawat 100 kama atazalisha 150 alipwe kwa hizohizo alizozalisha kutokana na utaratibu huu kama ukifuata kutakuwa na ushindani mkubwa kila mmoja atakuwa anajitahidi ili amzidi mwenzake sio huu wa sasa uzalishe usizalishe hesabu yako imeingia Tanesco hebu jaribuni maoni haya ya mlalahoi yatawasaidieni
 
Ngoja tusubiri mkataba na mrithi wa DOWANS tuone utakuwaje,ufisadi bado unaendelea yaliyofanyika IPTL ununuzi wa mafuta ni ufisadi pia,why tanzania always everything ufisadi?
 
wanajua sana ila kusudi ukizingatia kila matatizo yanapotokea wenyewe hayawakuti kivumbi sisi walalahoi,halafu nahisi masikio hawana na macho pia ndio maana wajifanyia mambo kiholela.mwishowe tunabeba mzigo taifa zima kwa ujinga wa watu wachache:mod:
 
Naomba nielekeze kidogo

Katika mikataba hii ya sasa lazima upige 'capacity charge' hii inalipwa whether amezalisha, yuko idle, anakarabatiwa etc...lengo ni kuencourage investors,

Unaweza kuleta mtambo wa hela nyingi sana lakini muda uliouleta TANESCO mabwawa yamejaa na wanazalisha bila kuhitaji ziada labda kwaajili ya 'voltage improvement' tu! So kujilinda na hasara capacitY charge inawekwa...

Angalizo...si TZ tu..ni kote ulimwenguni!
 
Back
Top Bottom