viatu virefu
Senior Member
- May 25, 2015
- 165
- 20
TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA UMEME KWA BAADHI YA MIKOA ILIYOUNGWA KWENYE GRIDI YA TAIFA FEBRUARI 27 NA 28, 2016
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake wa mikoa ya Singida, Shinyanga, Tabora, Mwanza, Musoma, Mara, Manyara, Simiyu na baadhi ya maeneo ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga kuwa yatakosa umeme siku ya Jumamosi na Jumapili Februari 27 na 28, 2016 kuanzia saa 2.00asubuhi hadi saa 11.00jioni.
SABABU: Kumruhusu Mkandarasi anayejenga Njia Kuu ya Kusafirisha Umeme ya Msongo Mkubwa ya Kilovolti 400 maarufu kama Backbone kutoka Iringa kwenda Shinyanga, kuendelea na kazi ya kuunga njia hiyo eneo la Mtera na kwenye vituo vya Kupooza na Kusambaza Umeme vya Iringa, Dodoma, Singida na Shinyanga.
Mradi wa huo wa Backbone unalenga kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini na utekelezaji wake upo katika hatua za mwisho.
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu.