TANESCO yaomba radhi umeme kukatika mara kwa mara Lindi na Mtwara, yasema kuna kazi ya kufunga Mifumo Mipya

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,891
13,644
Siku chache baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kuelezea kuhusu kero ya kukatika kwa umeme mara kwa mara Wilayani Masasi Mkoani Lindi, kusoma zaidi bofya hapa ~ Wakazi wa Masasi tuna kero ya umeme kukatika mara kwa mara, tunapata hasara TANESCO shughulikieni hilo , Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeomba radhi na kutoa ufafanuzi.

Snapinsta.app_468901362_18467935576065303_344741081158865179_n_1080.jpg


TANESCO MAKAO MAKUU, S.L.P. 453, DODOΜΑ, ΤΑΝΖΑΝIA, SIMU 0748550000

TAARIFA KWA WATEJA WA MIKOA YA LINDI NA MTWARA

Ijumaa, 29 Novemba, 2024.
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Mikoa ya Lindi na Mtwara kuhusu kazi ya kufunga mifumo mipya ya kuendesha mitambo kwenye Kituo cha kufua umeme kwa Gesi Asilia cha Mtwara.

Kazi hii, inatekelezwa na Mkandarasi TELENET kutoka Croatia, ilianza rasmi tarehe 10 Oktoba 2024 na inatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 12 Disemba 2024. Utekelezaji wa kazi hii umepelekea baadhi ya wateja wa Mikoa ya Lindi na Mtwara kuathirika na upatikanaji wa huduma ya umeme kwa nyakati tofauti.

Shirika limeweka mkazo mkubwa kuhakikisha kazi hii inatekelezwa kwa ufanisi na kukamilika kwa muda uliopangwa ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme kwa wateja katika Mikoa hiyo.

TANESCO inaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza kwa wateja katika mikoa tajwa wakati wa utekelezaji wa kazi hii muhimu.

Imetolewa Na;
KURUGENZI YA MAWASILIANO NA UHUSIANO KWA UMMA,
TANESCO-MAKAO MAKUU.
DODOMA
 
Wajifunze pia kutoa fidia kwa usumbufu za biashara za watu kutaa radhi haitoshì tu.
 
Back
Top Bottom