TANESCO: Taarifa ya hitilafu ya umeme jiji la Dar es Salaam

DAVID ROUBEN

Member
Joined
May 25, 2015
Posts
91
Reaction score
4
TAARIFA YA HITILAFU ZA UMEME ZILIZOSABABISHWA NA MVUA ZILIZONYESHA KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM TAREHE 5 NOVEMBA 2015

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kutoa taarifa kwamba maeneo kadhaa ya jiji la Dar es Salaam yalipata tatizo la umeme kutokana na mvua kubwa na upepo zilizonyesha katika jiji la Dar es Salaam kuanzia majira ya saa tatu asubuhi.

Pamoja na ukweli kwamba Shirika lilikuwa limewaweka tayari mafundi katika mikoa yote kukabiliana na tatizo lo lote la umeme, hali hiyo ya mvua ilifanya umeme kukatika katika maeneo mengi.

Baadhi ya maeneo yaliyoadhirika na hali hiyo kwa vipindi tofauti ni pamoja na Temeke, Kigamboni, Mbagala hadi Mkuranga na Chang'ombe baada ya gari kugonga nguzo ya umeme katika eneo la Mkuranga na upepo mkali kuezua bati kutoka kwenye jengo katika eneo la Shauri moyo na kulirusha juu ya line ya umeme inayoanzia Ilala hadi Mkuranga.

Eneo lingine ni Mandela Road hadi Tabata baada ya mvua na upepo kusababisha wire kukatika katika kwa span mbili eneo la LandMark Hotel.

Eneo lingine ni Kimara hadi Kibamba kutokana na Transformer iliyolipuka eneo la Kimara na nguzo mbili za line kubwa zilizoanguka kutokana na mvua.

Eneo la kati kati ya jiji lilipata hitilafu ya muda mfupi baada ya upepo mkali kudondosha kamba inayotumika kwenye ujenzi kutoka jengo linalojengwa karibu na yaliyokuwa makao makuu ya NMB na kudondoka kwenye line ya umeme ya C8.

Wateja wanaopatia umeme kutoka kituo cha Mbezi waliathirika na tatizo la Cable ya 33kV na d.c supply kwenye kituo hicho. Maeneo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo kikuu cha Ardhi, Makongo, Mwenge na Changanyikeni yaliathirika kwa muda.

Mafundi wetu walifanya jitihada kubwa japo katika mazingira ya mvua kurekebisha matatizo hayo katika muda mfupi kadiri ilivyowezekana.

Pamoja na changamoto hii, tunapenda kuwahakikishia wateja wetu nchi nzima kwamba hali ya umeme imeendelea kuimarika na umeme umekuwa ukipatikana nchi nzima ukiacha hitilafu ndogo za hapa na pale za kiufundi.

Kulingana na tahadhari zilizotangulia kutolewa na mamlaka ya hali ya hewa huenda mvua hizi zilizoanza zikaendelea kwa muda mrefu hivyo tunawaomba ushirikiano kutoka kwa wananchi katika kukabiliana na adhari kama hizi.

Tunawaomba radhi wateja wote walioathiriwa na hali hii.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

Zikinyesha mvua hitilafu....likiwaka jua kukauka kwa mabwawa
 
Shida yenu ni kuchelewa kutoa taarifa
 
sis sio wateja wenu, ninyi ndio wateja umeme huu ni wetu. tumewapa dhamana tu.

kujitetea huku ni tija kweli? umeme unapokatika tuseme nguzo au wire, au transforma hivi vitu kwa nn hamuweki vya akina, na standby service.

ni kwamba ndani muda mfupi baada ya tatizo umeme irejee sio mnakuja na maneno maneno
 
Ndio maana kuna kitu kinaitwa Technology Advancement. Hivi hizi sababu dunia.ya.leo ya tatu kama mexico hazisikiki tena
 
Mlilalamika mabwawa hayana maji imekuja mvua kuyajaza
 
Nguzo na nyaya za umeme wa tanesco zimeoza hata manyunyu na upepo kidogo eti inaharibu miundo mbinu
 
TAARIFA YA HITILAFU ZA UMEME ZILIZOSABABISHWA NA MVUA ZILIZONYESHA KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM TAREHE 5 NOVEMBA 2015

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kutoa taarifa kwamba maeneo kadhaa ya jiji la Dar es Salaam yalipata tatizo la umeme kutokana na mvua kubwa na upepo zilizonyesha katika jiji la Dar es Salaam kuanzia majira ya saa tatu asubuhi.

Pamoja na ukweli kwamba Shirika lilikuwa limewaweka tayari mafundi katika mikoa yote kukabiliana na tatizo lo lote la umeme, hali hiyo ya mvua ilifanya umeme kukatika katika maeneo mengi.

Baadhi ya maeneo yaliyoadhirika na hali hiyo kwa vipindi tofauti ni pamoja na Temeke, Kigamboni, Mbagala hadi Mkuranga na Chang'ombe baada ya gari kugonga nguzo ya umeme katika eneo la Mkuranga na upepo mkali kuezua bati kutoka kwenye jengo katika eneo la Shauri moyo na kulirusha juu ya line ya umeme inayoanzia Ilala hadi Mkuranga.

Eneo lingine ni Mandela Road hadi Tabata baada ya mvua na upepo kusababisha wire kukatika katika kwa span mbili eneo la LandMark Hotel.

Eneo lingine ni Kimara hadi Kibamba kutokana na Transformer iliyolipuka eneo la Kimara na nguzo mbili za line kubwa zilizoanguka kutokana na mvua.

Eneo la kati kati ya jiji lilipata hitilafu ya muda mfupi baada ya upepo mkali kudondosha kamba inayotumika kwenye ujenzi kutoka jengo linalojengwa karibu na yaliyokuwa makao makuu ya NMB na kudondoka kwenye line ya umeme ya C8.

Wateja wanaopatia umeme kutoka kituo cha Mbezi waliathirika na tatizo la Cable ya 33kV na d.c supply kwenye kituo hicho. Maeneo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo kikuu cha Ardhi, Makongo, Mwenge na Changanyikeni yaliathirika kwa muda.

Mafundi wetu walifanya jitihada kubwa japo katika mazingira ya mvua kurekebisha matatizo hayo katika muda mfupi kadiri ilivyowezekana.

Pamoja na changamoto hii, tunapenda kuwahakikishia wateja wetu nchi nzima kwamba hali ya umeme imeendelea kuimarika na umeme umekuwa ukipatikana nchi nzima ukiacha hitilafu ndogo za hapa na pale za kiufundi.

Kulingana na tahadhari zilizotangulia kutolewa na mamlaka ya hali ya hewa huenda mvua hizi zilizoanza zikaendelea kwa muda mrefu hivyo tunawaomba ushirikiano kutoka kwa wananchi katika kukabiliana na adhari kama hizi.

Tunawaomba radhi wateja wote walioathiriwa na hali hii.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao
 
Tunasubiri tu Dr. Magufuli awafukuze kazi hapo Tanesco, haiwezekani rais anaapishwa nyie mnakata Umeme ili wananchi wasishuhudie tukio hilo la kihistoria
 
Nyie wote mtafukuzwa kazi, tuanzishe shirika jipya maana hakuna namna nyingine
 
Nguzo na nyaya za umeme wa tanesco zimeoza hata manyunyu na upepo kidogo eti inaharibu miundo mbinu
Nimsikia wakisema wanabadilisha mfumo toka kwa nguzo za miti hadi kwenye nguzo za "concrete", ngoja tuone nayo kama itakuwa na matatizo au italeta suluhu..
 
Taarifa kama hii ilitakiwa ije mapema kwani umeme ulikuwa unakatika na kurudi. Hii itakuwa imesababisha hasara kubwa na kuharibu vitu vya watu.
 
Back
Top Bottom