TANESCO Rushwa imekithiri! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANESCO Rushwa imekithiri!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PMNBuko, Jun 10, 2012.

 1. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa miaka mingi sana nimekuwa nikisikia namna watanzania wanavyohujumiwa na shirika lao la umma, Tanesco. Leo yamenikuta. Baada ya kulipia gharama zote za kuunganishiwa huduma ya umeme kwa zaidi ya miezi mitano bila kupewa huduma husika kwa kisingizio kuwa hakuna nyaya, hakuna mita na juzi kuambiwa kuwa mita zipo lakini hakuna box za mita, leo nimetoa kidogo ndipo nimeunganishiwa umeme tena siku ya jumapili. Nimeumia sana kutoa rushwa. Lini Tanesco wataanza kutoa huduma stahili?
   
 2. MJIMPYA

  MJIMPYA JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45

  Wataacha siku wote tukiacha kutoa rushwa, tatizo tunapenda kulaumu wengine bila kujiangalia wenyewe.

  Kama kweli unapenda haki lazima ukubali machungu yake nayo ni kufuatilia bila kuchoka na kutokubali kutoa rushwa

  Mtoaji na mpokea rushwa wote ni mafisadi kwa sheria zetu.
   
 3. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,026
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  tanesco bila rushwa haiwezekani...wale jamaa wana njaa sijawahi kuona..ukiwa na chochote wanafanya faster mkuu,me ilinichukua wiki moja tu....
   
 4. k

  katitu JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 215
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Lakini fahamu na wewe umechangia kueneza rushwa tanesco.hukupaswa kutoa rushwa bali kufuata njia sahihi ya kudai haki yako hivyo na wewe ungekuwa tanesco unchukua rushwa.hivyo unatafutwa wewe na huyo jamaa yako wa tanesco uliyempa rushwa ili wote mfuguliwe mashitaka ya kutoa na kupokea rushwa.jamaa yangu hapa umeonyeha udhaifu mkubwa.umeshindwa kupambana na rushwa na badala yake unatoa rushwa.
   
 5. BIG Banned

  BIG Banned JF-Expert Member

  #5
  Jun 10, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 263
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wamezoea hivyo, lakini na sisi tunawaendekeza kwa kuwapa rushwa. Ungewakamatisha kwa takukuru.
   
 6. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waweza kunilaumu lakini ukweli ni kwamba hawa jamaa hawajawahi kuunganisha umeme bila rushwa hasa huku mikoani. Tanesco ni janga. Nilikaa kimya miezi mingi nikitafuta haki nikachoka.
   
 7. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu pole kwa yaliyokukuta. TANESCO ni janga la kitaifa kwa rushwa. Unaweza kugoma kutoa rushwa lakini ujue itakuchukua muda mrefu kupata hiyo huduma. Inanikumbusha mwaka jana nilivyogombana nao kwa kuchelewa kuja kuniwekea mita ya luku ambayo nilikuwa nimeilipia mwenyewe. Hawa jamaa walikuwa na kawaida ya kupita kwangu na kukata umeme kila sikukuu kubwa kama Pasaka, Idd na Xmas zinapokaribia. Wakifika wanakata tu bila kuuliza kama tumeishalipia bili yetu ya mwisho. Kwa kujua tabia yao ilipokaribia Xmas mwaka jana nikaenda nikaomba bili yangu nikalipa kabisa. Tarehe 23.12.2011 jamaa wakapita wakakata kama kawaida. Nikaenda pale magomeni kuwauliza kwanini wamenikatia umeme bila hata kuulizia kama nimelipa? Hawakuwa na majibu ya maana hivyo nikaomba niwekewe mita ya LuKU. Wakanitaka nilipie Tshs. 30,000 na kwamba mita itakuja kufungwa ndani ya wiki moja. Wiki ikapita, mwezi, miezi miwili ikapita nikaaanza kufuatilia wakawa wananiambia watakuja kufunga mpaka miezi minne ikapita.

  Siku nilipoamua, nilifuta suti yangu moja vumbi nikaitinga na kwenda kwa meneja pale magomeni. Nilipofika nikaomba kuonanana na manager lakini Secretary akanikatalia kwamba nimwambie yeye hilo tatizo langu. Nikamwambia sitamwambia mtu yoyote shida yangu isipokuwa manager. Akasisitiza kwamba nikimwambia shida yangu atanielekeza kwa mtu ambaye ataweza kunishughulikia. Wakati tunaendelea kubishana manager kule ndani akasikia akatoka kuja kujua kulikoni. Akanikaribisha ofisini kwake nikatoa list ya malipo nikamwuuliza kwanini sijafungiwa mita kwa siku zote hizo. Wakati huo mita tayari zilikuwa zimeanza kufungwa bure. Alinyanyua simu akamuita Bwana mmoja aje ofisini kwake mara moja. Alipofika akamuuliza ni kwa nini hiyo mita ilikuwa haijafungwa jamaa akajaribu kujikanyaga manager akamwambia before closure of business that day atapenda apewe taarifa kwamba mita tayari imefungwa.

  Yes unaweza kuepeuka kutoa rushwa lakini kupata huduma uwe tayari kuchukua muda mrefu!!!!

  Tiba
   
Loading...