TANESCO: Rationing is back!


Mkuu huko kwenu utaanza? Sisi tunao kwa wastani wa mwezi na nusu hadi miwili sasa
 
Walikuwa wanatania mkuu
 
Pole sana boss...at least ujionee jinsi mambo yanavyokuwa tukiwa hatuna umeme
 

Ndo maana nikasema jk akifanya timua timua kwenye tanesco nae inaweza ikamhusu
 
Agizo hilo ni feki halina mshiko maana halikuangalia source ya tatizo,tatizo si William mhando,tatizo ni serikali ya magamba kutokuwa na mipango mkakati wa kuimarisha sekta hii ya Umeme,tangu awamu ya kwamza mabwawa ya maji yalipotengenezwa hakuna serikali zilizofuata kuweka mipango ya kuimarisha sekta hii!
 

mamilioni haya kibao yanayokopwa kila kucha na tenesco kutoka taasisi kibao cha nchi za ulaya zitalipwaje jamani ??
Ni hatari sana kwa mkurugenzi kuanza kujifikiria yeye kwanza huku wateja wanaompa chakula wakiwa hawana uwezo wa kupata umeme. mtu mbinafsi san huyu.
 
Pia mimi nashauri haya:

1. Waziri wa elimu naye aondolewe kwenye pay roll kama miezi miwili hivi ili ajue adha ya walimu wanaoondolewa kwenye pay roll kiuzembe halafu wanapata usumbufu mkubwa kurudishwa

Watoto wake AU Wajukuu lazima waandikishwe shule za kata
 

Wakuu hii issue ya tanesco imeshakuwa kama tamsilia ya isidingo the need!
 

Walipitisha bajeti kwa mbwembwe kama madereva wa bodaboda!This mzee wa megawats na Mzee mapete hamtoki ngoja session zianze!
 

Rais naye ajitimue kazi tufanye uchaguzi upya.
 
We are great thinkers let us think deeply, kwa maoni yangu mkurugenzi wa TANESCO wanamwonea. Yeye angekuwa ni chanzo cha tatizo ningekubaliana na hatua hiyo ya kukatika mara kwa mara kwa umeme. Namkubali Zitto lakini kwa hili kachemsha. Je, Mhando akienda kushitaki mahakamani kuwa mkataba wake wa kazi umekiukwa itakuwaje. Nafikiri ni bora wakaadhibiwa wale walioifikisha TANESCO hapa ilipo.
 

Mhando hizi story wananchi wamezichoka kila siku visingizio hivyo hivyo.
Mytake.
Mhando atawashtaki tanesco kwa kukiuka mkataba na atashinda kesi la ruling itailazimisha tanesco kumlipa hiyo damage.This country bwanaa!
 
Karibu gizani Kaka mkubwa, ili na wewe uonje uchungu wa kukatika kwa umeme mara kwa mara!
Tunajua una uwezo wa kureplace mara tu litakapo ondolewa, lakini utatumia mshahara wako kulihudumia ili uweze kutukumbuka sisi wanyoge!
 

Mbinu chafu??? Hakuna kitu kama hicho, kwani uchaguzi wa arumeru usipozungumziwa nini kitatokea? Kura zitapigwa na ccm lazima iangukie pua.

Suala hapa ni serikali dhaifu na viongozi waongo. Watuambie bajeti ya 1.2trillion ya umeme wa dharura na ile mipango iliyotangazwa na Pinda bungeni imeyeyukia wapi? Tungependa kuona rais na serikali yake inawajibika haraka. Nchi imeanza kuingia kwenye tatizo la mgao, na kwa hali ilivyo tatizo litakuwa kubwa zaidi ya ilivyokuwa mwaka jana. Kuna haja gani ya kuendelea kuiacha serikali hii iendelee kudidimiza uchumi wa nchi?
 
wapendwa,

binafsi nawashangaa wote mliojadili hapa, namshangaa mkurugenzi wa tanesco na pia mwenyekiti wake wa bodi!

kwani POAC ina mamlaka gani ya kuiamuru tanesco jambo lolote? mnajua maana ya separation of powers? hiyo POAC si ni ya upande wa uwakilishi (bunge) na tanesco upande wa utekelezaji (serikali). hebu tutafakari tena hapo!

ili kuwafunza adabu watu wavivu wa kufikiri, nashauri hilo generator likishaondona hapo, siku umeme ukikatika kwake tu, aende mahakamani mara moja, ili tujue kuwa bunge ni wasimamizi tu wa seriklali na hawawezi na wala hawana haki wala mamlaka yoyote ya "KUAGIZA' moja kwa moja lolote na likatendeka huko serikalini kwa mujibu wa katiba na sheria zetu.

kwa kweli zito na kamati yake walichemka, ila hawa watakaotekeleza watakuwa wamechemka zaidi!

mbarikiwe sana wapendwa

Glory to God!
 
Hapo hakuna atakachopoteza sana sana ni kumwonea tu! Kwa nini wasimguse hata Waziri mwenye dhamana na Katibu mkuu wa wizara ya NM? Hapa naona jamaa wanamwandalia mazingira ya kujilipa mamilioni.
 

Mkuu hata shambani kwa Sumaye kiluvywa ilipelekwa 11kva nani alilipia gharama hizi kule ulongoni Gongo la mboto kwenye wakazi zaidi ya elfu tatu umeme hakuna na watu tushalipa gharama za kuletea umeme haujaletwa mpaka tumeenda mahakamani ,

Rais dhaifu,hata viongozi wa mashirika watakuwa dhaifu wiki iliyopita Prof.Mbwete alikaririwa akisema wameingia mkataba na Mwizi wahela za OPEN UNIV.arudishe taratibu kama Rais alivyoingia mkataba na wezi wa EPA.
 
Kila siku TANESCO inadaiwa, pamoja na kupandisha bei ya umeme bado inadaiwa. Kama wameshaonesha kushindwa ni kwa nini tusitumie njia mbadala? Say, yaruhusiwe makampuni binafsi kuuza umeme kwa watumiaji!

Mkuu mimi naamini nchi hii bado ina watu wazuri wanaoweza kuongoza. Pia nafahamu kwamba huko TANESCO kuna viongozi wazuri tu tatizo ni siasa mkuu. Hivi kwa nini Dr. Idrissa aliondoka? Jibu ni kuingiliwa kisiasa. TANESCO ni shamba la bibi kila mtu anataka aingilie. Wanauziwa umeme bei aghari hawatengenezi faida! Watu wanakula kwenye mafuta ya kuendeshea mitambo ya IPTL! Mambo ni mengi.
 
Bora yajitokeze makampun mengine ya kuzalisha umeme.na Tanesco wabakie kumiliki nyaya na nguzo wao ndio wawe wanapiga servirse.

Iwe kama makampuni ya simu ingawa kila kampuni linamatatizo yake lakini siku zinasonga wakizingua tigo unawapiga chini unaweka voda wakizingua voda unahamia air tel nao wakileta magumashi yuleee zantel safari com na ttcl nao watakusubiri tu.

Lakini kwa hawa tanesco wanatuzingua sana kwanza bei zao ziko juu ukiachana na bei huduma ndiyo hizo magumashi mara washa mara zima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…