Kote huko Mboma anazunguka tu kukopa hakuisaidii Tanesco,wamekopa mara ngapi na hakuna ufanisi wowote,Tanesco si walisema wanaongeza bei ya umeme kuanzia January mwaka huu ili kuongezea hela ya uzalishaji sasa huko kukopa ni kwanini,sisi Tanzania umeme uko juu kuliko nchi zote katika EA.Tatizo ni Tanesco kulipia madeni kwa akina Dowans,IPTL,Songas na wengineo,wenyewe ndio wametuingiza kwenye mikataba mibovu,akina Mkapa na Net solution ,hela ya Tanesco ndio hiyo inayoenda kwenye harambee za makanisa,kwenye kampeni za Arumeru na ndio hizo zitamuingiza mtu Ikulu.
Inasikitisha kuwa mpaka sasa wakati tuna gesi asili kibao,tuna makaa ya mawe baado Tanesco wanalia na mvua.Hapo Kenya wenzetu wanachimba visima vya gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme na kampuni inayochimba ni ya umma na si wawekezaji wababaishaji,jamani hata Kenya wanatushinda?wao hawana mito wala gesi nyngi kulinganisha na sisi wala hata makaa hawana.pia pale Stiegler vipi.Huu mgawo ulianza enzi za Mwinyi mpaka sasa zaidi ya miaka 25 hakuna ufumbuzi.Tanesco inabidi igawanywe wawo wawe wasambazaji tu,iundwe kampuni ya umma ya kuzalisha umeme hao kazi yao iwe ni kuzalisha umeme tu,nendeni hapo Kenya mkajifunze!! sio kila mko safarini Ulaya wakati hapa jirani kuna shule tosha.NCHI HII INAKERA SANA BASI TU SAWA NA MTU HUWEZI KUWAKANA WAZAZI WAKO NDIO MAANA naona kukereka na UZEMBE huu wa miaka nenda miaka rudi