TANESCO nusura itoroshe watuhumiwa Temeke.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANESCO nusura itoroshe watuhumiwa Temeke..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by VUTA-NKUVUTE, Mar 28, 2012.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Jana nilikuwepo Mahakama ya Wilaya ya Temeke kuendelea na wajibu wangu wa kuwawakilisha wateja wangu kwenye mashauri yao.Mahakimu,waendesha mashtaka,makarani,askari polisi na magereza,watuhumiwa, na wananchi wa kawaida walikuwa 'bize' kutimiza wajibu wao.Mambo yalikuwa yakienda vyema.

  Ghafla,ikatokea hitilafu ya umeme.Vyumba vyote vya Mhakimu vikaathirika.Milio ya hatari ya umeme ulioshindwa kumilikiwa ikasikika.Kila mtu akawa anajitahidi kuokoa roho yake.Mahakimu,Makarani,Mawakili,na wananchi wakakanyagana wakikimbia.Kama filamu vile.Mchafukoge.

  Askari wakakumbuka kiapo chao cha kutokuwa waoga.Wao walibaki.Walibaki kuwadhibiti watuhumiwa wa ndani(waliotokea mahabusu) iliwasitoroke.Wakawadhibiti.Wengine walishafika Uwanja wa Taifa,wengine mbali zaidi.

  TANESCO ijitahidi hali kama ile isitokee tena..
   
Loading...