Tanesco na ufungaji mita mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco na ufungaji mita mpya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MduduWashawasha, Jul 1, 2012.

 1. MduduWashawasha

  MduduWashawasha JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 1,568
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Habari wana JF.kuna kitu kimekuwa kikinishangaza wakati nakisikia kwa watu na sasa kinanitokea na mimi.Hawa kampuni ya umeme wako ktk kazi ya kufunga mita mpya kwa wateja.Cha kushangaza unit 50 Wanazojuwekea zikiisha basi tarajia usumbufu mkali sana kwani hiyo meter itagoma kupokea umeme utakaonunua.Utahangaika na fundi aliyefunga, naye atakupa namba ya call center ambako mtasumbuana sana na hao jamaa kwa majibu ya ovyo.Mpaka mambo yarekebishwe amin nakuambia wiki moja au mbili utakaa bila umeme nyumbani kwako.Najiuliza hawa jamaa wana client service charter?na ndivyo inavyosema? kama ni kitu common kwann wasijipange jinsi ya kudeal na hili tatizo?inabore sana nchi hii sioni hata shirika moja la serikali lunalofanya kazi kwa ufanisi
   
 2. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Mita yako aipo kwenye data base ya mita za Tanesco.vishoka wana mita zao ambazo azijasajiliwa Tanesco.system ya Mita za LUKU ni kuwa Vocha za Luku aziwezi kufanya kazi kwenye mita isiyosajiriwa na kampuni husika.Mfano mita ya Luku ya South Africa aiwezi pokea Units za Tanzania..Vishoka wanauwezo wa kuiprogram mita za luku zijiwashe zikiwa na unit ngapi let's say 50 units,wewe kwa furaha ya umeme utawamalizia chao,wakishaondoka wewe unabaki na maumivu.onana na meneja wa mkoa wako atakusaidia
   
 3. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  sasa itakuaje MUNGU wangu mwenzangu na mie wazee kule kijijini watafanyaje
   
 4. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Onana na meneja wa Tanesco mkoa wako mwambie ukweli,atakusaidia kuiweka mita yako kwenye database ya Tanesco baada ya hapo tatizo litakwisha,uende na serial Number ya mita yako ya luku. Kama uwezi iona ni PM ntakupa code ya kuifanya ikuonyeshe kwenye screen
   
 5. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2012
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  ...Uliipata kwa njia halali ama kupitia vishoka?? Nina kijana wangu amefungiwa mita ya Luku kama miezi miwili na nusu iliyopita. Toka zile unit 50 zilipokwisha hajawahi kukanyaga Ofisi ya Luku maana ananunua kwa simu tu na mambo yanajipa! Ya kwako itakuwa na tatizo. kama ulivyoshauriwa na wenzangu, kamuone Meneja wa Mkoa wako wa Tanesco.
   
Loading...