TANESCO: Na mvua zote hizi mpaka za mafuriko, kwanini bado kuna mgao wa umeme?

aggrey kimambo

Senior Member
Aug 10, 2015
129
142
Maajabu hayaniishi katika hili bado, TANESCO watoke hadharani waseme mgao wa umeme hausababishwagi na upungufu wa maji kwenye mabwawa yanayozalisha umeme, bali ni vitu vingine. Na wavitaje hivyo visababishi vingine maana imeshajidhihirisha siyo upungufu wa maji. Maana mvua zote hizi mpaka za mafuriko tulitegemea kusiwe na mgao hata kidogo wa umeme.

Kwamfano huku moshi leo umeme upo, kesho haupo siku nzima,(na ni continious circle)hili swala linatuathiri sisi wafanyabiashara wadogo tunaotegemea umeme kama mainbody ya biashara. Tanesco acheni figisu figisu bhana, TRA wanakomaa wanatufungia maduka, bidhaa hazinunuliki, pesa imekuwa ngumu na TANESCO nao wanaleta figisu.

Huo utumbuaji wa majipu uwe na faida kwetu sisi wananchi wa kawaida kwenye kufanya Urahisi wa maisha, kama utumbuaji huo unaendana na hali ya maisha kuzidi kuwa ngumu kwetu, TUTACHOKA.

TANZANIA NCHI YA KUFIKIRIKA.
 
Pole sana mkuu kwa tatizo lakini Miundo mbinu ya kusafirisha umeme si rafiki sana na mazingira haswa kwa umeme wa msongo wa kati 33 na 11KV nguzo hudodoshwa sana na mvua hizo hivo kupelekea breakdown na kufanyika maintenance ndo hu cost umeme kukatika, Maji ni fact ndogo sana japo asilimia karibu 54 ya umeme hutokana na maji, plant zinafua sasa mbinde nu kusafirisha
 
Back
Top Bottom