TANESCO mna nini na Ukonga-Kipunguni?

TANESCO mna nini na Ukonga-Kipunguni?

JOYSTICK

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2014
Posts
221
Reaction score
57
TANESCO hata kabla ya kutangaza kuwa mtakata umeme kwa wiki mbili mfululizo kwetu huku mlikuwa mnakata bila hata taarifa lakini kibongo bongo tunavumilia.Sasa ilivoanza hizi wiki 2 ndo imekuwa shida maana mnakata toka saa moja asubuhi mpaka saa6 usiku ndio mnarudisha wakati huo pale Banana na maeneo mengine umeme upo,ukipigia marafiki wanaokaa maeneo mengine wanakwambia umeme umerudi Kipunguni umeme bado.Jamani kwanini?

Kuna nini Kipunguni mnatuonea hivo kila siku umeme unakatwa tu hukuu tena masaa mengi zaidi ya sehem zingine?Kwanini au kuna mbaya wenu mnataka kumkomoa au maana kiukweli ni kilio cha wakazi wote wa Ukonga Kipunguni.

Tafadhali jirekebishen maana huu ni uonevu.
 
Gnassingbe usiwe na mawazo mgando usichanganye siasa na Tanesco kwani Tanesco nishilika la uma na haliusiki na chama chochote cha siasa. Na kupotosho uma ili ionekane Tanesco ni mbaya pia ni makoso. Tambua hiki ni kipindi cha mpito tu na baada ya hapa kilakitu kitarudi katika hali yake
 
Gnasssingbe acha masihala bana ccm kwan inauhusiano gan na TAnesco????

Acha kutufanya wenzako hatujasoma
 
Mchagueni mbunge mwita mwikabe yuko sharp kwa kufuatilia mambo
 
Mwana unapiga chapua hapahapa, au kwenye mgao na wewe umo?

Basi haya
 
Yaani nyie mnakatiwa masaa 6 mnalalamika...wenzenu huku masaa 12.... kama hapa washakata tayari ngoma hii hadi kesho saa moja na nusu saa mbili

Anyway kimgao chao wamekiongezea tarehe? Nikidhani kinaisha tar 14???
 
Hata na kwetu Kijichi ndiyo tuko hali mbaya kuliko hata nyinyi huko Kipunguni.

Takriban kila siku umeme unakatwa, tena kwa masaa yasiyokuwa na idadi. Siku nyengine unarudi hauna nguvu kabisa.
 
Mkuu nafikiri hiyo line ya Kipunguni ni sawa na Mongolandege. Jirani zetu Kinyerezi tunaotenganishwa na mto tu kwao full umeme. Ila sisi wa upande wa pili ni kateso kweli. Hili shirika ni kati ya mashirika yanayofanya wananchi kuchukia serikali.
 
Gnasssingbe acha masihala bana ccm kwan inauhusiano gan na TAnesco????

Acha kutufanya wenzako hatujasoma

Ccm ndio inatawala nchi,chochote kinachotokea kiwe kibaya au kizuri anaelaumiwa ni ccm. Kwani mkurugenzi wa tanesco anajiteua mwenyewe au anateeuliwa na rais wa ccm?
 
Gnassingbe usiwe na mawazo mgando usichanganye siasa na Tanesco kwani Tanesco nishilika la uma na haliusiki na chama chochote cha siasa. Na kupotosho uma ili ionekane Tanesco ni mbaya pia ni makoso. Tambua hiki ni kipindi cha mpito tu na baada ya hapa kilakitu kitarudi katika hali yake
Kwani mkurugennzi wa tanesco na bodi ya tanesco wanajiteua wenyewe au wanateuliwa na rais wa ccm.

Ccm ndio inaandaa sera na kuiambia tanesco itekeleze,sio wao wanajipangia kwa hiyo ccm hawachomoki kwa hili ndio
 
Tayari washkata tena.....

Yaani kijichi ni shida.......

Ila tukome kuichagua ccm

Hata na kwetu Kijichi ndiyo tuko hali mbaya kuliko hata nyinyi huko Kipunguni.

Takriban kila siku umeme unakatwa, tena kwa masaa yasiyokuwa na idadi. Siku nyengine unarudi hauna nguvu kabisa.
 
Back
Top Bottom