TANESCO mkoa wa Iringa mna shida gani? Kwanini kila siku kata ya Ifunda inakosa umeme?

PyongZhong

Member
Jun 19, 2020
9
45
Tangu tarehe 1 mwezi wa 1, wana Nchi walisherekea sikukuu ya mwaka mpya bila umeme. Umeme ulikata kuanzia saa saa 12 jioni, mpaka saa 4 usiku ndiyo mkarudisha.

Tangu tarehe moja mwezi huu, mpaka leo hii tarehe 7, mmekuwa mnakata umeme kila siku. Mna kata umeme saa 2 asubuhi au saa 8 mchana, mnarudisha saa 3 au saa 4 usiku.

Yaani kuanzia saa 4 usiku mpaka asubuhi umeme una kuwepo, ila asubuhi na mchana mnakata umeme muda wowote ule, iwe kuna mvua au kuna jua. Je, umeme ni wa mgao?

Wakati huo huo Ifunda ikiwa haina umeme, Iringa mjini na Mafinga mjini, umeme una kuwepo muda wote.

Hata kama mtakata Iringa mjini na Mafinga mjini basi lazima mtatoa taarifa, na kama mkikata bila kutoa taarifa, basi mnakata ndani ya nusu saa umeme mnarudisha. Kwani nyie mna upendeleo?

Kata ya Ifunda na kata zinazo izunguka Ifunda zimewakosea nini? Imekuwa desturi sasa kwa TANESCO kufanya haya.

Meneja wa umeme wa mkoa wa Iringa unakwama wapi? Kwanini kila siku kata ya Ifunda na Vijiji vinavyo izunguka vinakosa umeme na kukaa kwenye giza ikiwa wateja wenu wanalipia?

Naomba kuwasalisha. Hii ni kero kwa wana Nchi.
 

Kamkuki

JF-Expert Member
Feb 1, 2011
1,489
2,000
Dar penyewe tuna mgao
Umeme unazimwa Asubuhi kwenye saa 2 Ivi na kurudi tegemea kuanzia saa kumi hadi 12 jioniii
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom