TANESCO kushusha umeme kumesaidia wateja wa kawaida au bado hali ya umeme ipo pale pale?

Come27

JF-Expert Member
Dec 1, 2012
7,693
7,357
JE UNAFAHAMU KUWA TANESCO IMEPUNGUZA BEI YA UMEME NA KUONDOA TOZO YA KUTOA HUDUMA (SERVICE CHARGE) KWA WATEJA WA T1 KAMA ILIVYOONYWESHWA KWENYE JENDWALI HAPO CHINI KUANZIA TAREHE 1/4/2016. UMEJIPANGAJE KUTUMIA FURSA HII KUKUZA UCHUMI WAKO BINAFSI NA WA TAIFA?
 
Well tunashukuru sana kwa hatua hii ya gharama za kulipa ankara ya umeme kupunguzwa, nimeona effect yake ambayo kwangu ni chanya kwani kazi zangu zinagharimu sana umeme.
 
Jamani Nina wasiwasi na utekelezaji wa hili swala la kupunguza bei. Juzi jamaa yangu aliniomba nimnunulie umeme na hiki ndicho kilichotokea

Ref CB49UV657
01......(nimefuta namba)
Rcpt MAXCO33EMDB45005720
Units 28.1KWH

Token 1274 7393 8828 3129 1162

Cost TZS 8196.73
Serv Charge TZS 0.00
Tax TZS 1803.27
Total TZS 10000
eSign
 
Mwezi wa tatu Huyu mtu alinunua umeme na alikatwa service chaji.

Kiwango cha units kilichopatikana kwa sh. 10000 ni kilekile kilichokuwa kikipatikana miezi ya nyuma.

Tofauti na matarajia yangu sikuona Mabadiliko katika gharama. Sijui tatizo liko wapi?

Kwa nikigawanya gharama ya unit is (baada ya kuondoa kodi) napata bei ya sh. 291.6 kwa unit. Mwenye kuelewa mahesabu ya tanaseco anisaidie
 
Hata kwetu bado tunachajiwa kama zaman, no changes sijajua shida ni nn
 
Mabadiliko yapo,kwa mwezi hua nanunua umeme wa alfu 40 lkn mtindo wa alfu 20, ukiisha na nunua tena 20. Lkn kwa mwezi huu nahisi sitaweza nunua hivyo maana nilipo nununua last week nilipata unit 56.2 kwa alfu 20 badala ya unit 36 za awali..
Hapana nahisi nitaongeza wa aldu 10 tu nitoboe mwezi.
 
Wametoa service charge ila kimsingi bei bado sio rafiki kwa mwananchi wa kawaida,
 
Tatizo lililopo apa Tanzania kwetu viongozi washazoea kutudanganya sana sasa ivi wanasema kwamba umeme wa D1 kwa kuanzia 0-75Units analipa Tshs 100. Alafu ktk D1 matumizi ya zaidi ya 75kwh wanachajiwa 350 Tshs @Unit. Lakini watu wakinunua umeme wanachajiwa 355.87. Sasa apo swali linakuja ilo 5.87 ni VAT au hata siielewi. Yaani Jamaa wanazingua sana
 
496744313977757258928cfd90f7ecd1.jpg
 
Back
Top Bottom