TANESCO kupinga malipo ya DOWANS mahakamani

Wahusika wote hawa wa Richmond wako serikalini ama wanalindwa na viongozi wa serikali, nao ijumaa wataadimisha kumbu kumbu ya miaka 12 ya Mwl Nyerere - unafiki mtupu. Hata sitta aliyeongoza kuvunjwa kwa mkataba wa Richmond/Downs naye anapinga malipo, wakati haya ni matokeo ya maamuzi yake. Kweli Tanzania tuko pabaya kuliko wakati wowote tangu tupate uhuru.
 
Tanzania ni miongoni mwa nchi masikini sana duniani. Hizo ni fedha nyingi sana kuwahi kudaiwa nchi hii. Ni vigumu sana kuepuka kuzilipa isipokuwa tu kwa miujiza tena ya ajabu. Madhara ya kuchelewa kulipa ni makubwa mno! 7.5% ya bil 94 siyo mchezo! Serikali inalazimika kulipa haraka iwezekanavyo kuepuka madhara zaidi. Nawashangaa sana wanasheria mahiri waliopendekeza na kushadadia kuvunja mkataba wa dowans, sijui wamesoma wapi sheria hadi wakapata PHD...!? nashangaa sana..! Nashangazwa zaidi na bunge la 'viwango...!' lililokuwa na spika mwanasheria kushindwa kugundua athari za kuvunja mkataba huo. Haizekani kukataa kwamba wahusika walikua wakitaka kujizolea umaarufu. Narejea matukio "tatizo siyo Richmond, tatizo ni Uwaziri Mkuu" nashawishika kuamini tatizo lilikuwa hilo.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…