TANESCO: Kukosekana kwa umeme kwa baadhi ya maeneo yaliyoungwa grid ya taifa

pinpilojr

Member
Jul 8, 2015
59
10
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)


TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA UMEME KWA BAADHI YA MIKOA ILIYOUNGWA KWENYE GRIDI YA TAIFA JUNI 26, 2016


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake wa Mikoa ya Dodoma, Singida, Shinyanga, Tabora, Mwanza, Musoma, Mara, Babati, Simiyu na baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga, kuwa yatakosa umeme siku ya Jumapili Juni 26, 2016 kuanzia saa 1.00 Asubuhi hadi saa 9.00 Alasiri.

SABABU: Kuruhusu Mafundi kutatua tatizo la dharura lililojitokeza katika Kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha Dodoma.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na; Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
 
Back
Top Bottom