nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,803
[h=2][/h]JUMATANO, JANUARI 09, 2013 06:52 NA GABRIEL MUSHI, DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amesema mwaka huu lazima alifumue Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kulisuka upya ili kukidhi mahitaji ya umeme.
Pia alisema Serikali, haitakubali kupandisha bei za umeme hadi hapo mapato na matumizi ya shirika hilo yatakapofanyiwa ukaguzi na kujiridhisha.
Profesa Muhongo, alitoa kauli hiyo mjini Dar es Salaam juzi, wakati akizungumza katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV mjini Dar es Salaam juzi.
Alisema msimamo wa Serikali, hadi sasa ni kwamba bei ya umeme haitapanda.
Ewura na TANESCO, wamefuata taratibu zao za kubadilisha bei, lakini nimewaeleza na narudia kusisitiza chochote watakachojadili labda waje na bei ya kushusha umeme Serikali haikubali bei ya kupandisha umeme huo ndio msimamo haubadiliki.
Bei haitapanda, nimewaambia Tanesco kwamba endapo wanataka kupandisha bei ni lazima tukae chini na wao tuangalie matumizi yao ya fedha wanazozikusanya, sasa ikiwa kama matumizi yao ni makubwa hayaendani na hali halisi cha kwanza ni kufumua hilo shirika la Tanesco, nashukuru Watanzania walitoa maoni yao kuhusu muundo wa shirika wanalolitaka sasa yamekusanywa na wiki hii tutaletewa wizarani.
Ujumbe wa mwaka wa 2013, ni lazima tufumue TANESCO tujenge upya ambayo itakidhi mahitaji yetu ya leo ya umeme, tunaotaka leo hii ni ule ambao utahakikisha uchumi wetu unakua kwa kasi zaidi, huwa unakua kwa asilimia 6.7, lakini tukitaka kupunguza umaskini ni lazima ukue kwa asilimia 8 hadi 10. Tukitaka ukue TANESCO ya sasa hivi haikidhi, lazima tuifumue huenda tutakuwa na kampuni moja mbili au tatu, nawahakikishia lazima tuwe na shirika na muundo mpya, inatupatia umeme wa uhakika, unaotabirika wa kuendesha uchumi wetu.
Lakini pia mgawo wa umeme haupo na hautakuwapo, ndiyo maana sikubaliani na mawazo ya TANESCO na EWURA ya kupandisha umeme, kwa sababu fedha ambazo zinatumika kufua na kusafirisha umeme sasa hivi, ni fedha ambazo zinatokana na kodi za Watanzania.
Fedha hazitoki TANESCO, wala EWURA hivyo hakuna sababu ya msingi mtu ambaye anazalisha umeme kwa kutumia hela yake alafu umpandishie bei, pia suala la mgawo halipo na nimewaeleza kwamba umeme wetu ambao tunautumia kwa wingi sasa hivi unatokana na gesi asilia, ni kati ya asilimia 40 mpaka 70, unategemea ni wakati upi tunachukua hizo takwimu, kwa hiyo umeme wetu mwingi hautokani na maji, kwa hiyo kina cha maji kishuke chini kiasi gani umeme wetu unatokana na gesi.
Tunapaswa tutambue, miundombinu ya kuzalisha na kusambaza umeme imechoka, mashirika mawili yaliyoitengeneza TANESCO yetu hii yalikuja kwa pamoja mwaka 1930. Kwa hiyo tangu enzi ya ukoloni, miundombinu hii haijabadilishwa ndio maana ikitokea hitilafu Ilala, jiji zima linaweza kukosa umeme.
Kinachofanyika sasa, ni kujaribu kuifanya iwe ya kisasa, kwa mfano katika hayo matengenezo inatokea kwamba umeme inabidi uzimwe sehemu fulani ndipo watu wanasema ni mgawo hapana sio mgawo... Watanzania, tunapaswa kuamua kama tunataka miundombinu yetu iboreshwe na wakati wa kuboreshwa lazima umeme uzimwe au tunataka kubaki na miundombinu ambayo mingine imekuwapo enzi ya ukoloni? Ni afadhali tuvumilie umeme uwe unazimwa ili tuboreshe miundombinu yetu, alisema.
MSIMAMO WA GESI
Pamoja na mambo mengine, Profesa Muhongo amesisitiza kuwa wakazi wa Mtwara mjini na wasomi wanapaswa kutambua gesi asilia, inayozalishwa kutoka ndani ya bahari ya Hindi ukanda wa kusini sio ya mikoa ya Mtwara na Lindi, kwani Katiba inaonesha mipaka ni ya Watanzania wote.
Alisema wanaowapotosha wananchi wa Mtwara kwa kutaka kuvuruga amani, wakati wanafahamu gesi hiyo ilitengenezeka miaka milioni 199.6 hadi milioni 23.03, kipindi ambacho mipaka haikuwapo.
Alisema wasomi wanaoratibu maandamano ya wananchi kupinga bomba la gesi kwenda Dar es Salaam, hawaelewi vitu kwa sababu ndani ya Mkoa wa Mtwara, kutajengwa kiwanda kikubwa cha kusindika gesi asilia (LAG) na kiwanda cha mbolea na saruji.
Vilevile tunapaswa kufahamu, tuna ushindani na mataifa mengine, kwa mfano Kenya wamegundua mafuta kule Ziwa Turkana, Uganda pia wamegundua ujazo wa mapipa bilioni mbili, Msumbiji ndio hao wamegundua gesi asilia zaidi yetu na Somali ikitulia pia wanaweza kugundua zaidi.
Kwa maana hiyo, hata tukila siasa namna gani lazima tuweke maanani kwamba hata hawa wenye uwezo wa kuendelea kutafuta hiyo gesi asilia wanaweza kuhama, wakaenda sehemu iliyotulia.
Kwanza Katiba yetu, inaeleza kwa uwazi, rasilimali za Tanzania ni za Watanzania wote. Kwa hiyo anayekuja na dhana nyingine ya kutaka uchumi wetu uvunjike au ugawanyike kimikoa mikoa huyo anavunja Katiba na sheria ya nchi yetu. Kila kitu kipo wazi, hakuna maliasili ya mkoa fulani.
Ndio maana waliofanya maandamano kule Mtwara mjini, tena ajabu gesi haipatikana Mtwara mjini ni vijijini, hayo ndiyo mambo ambayo Mwalimu Nyerere alitueleza ukianza hii dhambi ya kubagua watu ni mbaya sana inaweza kukumaliza mwenyewe, kwa mfano hao wa Mtwara mjini hawana gesi ni upuuzi mtupu ni ya Mtwara vijijini. Watu wa Mtwara mjini inabidi wakubali kwamba gesi ni yetu wote kwa sababu nawao hawana hiyo gesi.
Tuna sheria ambazo zinatuongoza kugawa mipaka yetu kimikoa, sheria tulizonazo zinasema hivi... kwa mikoa ambayo iko karibu na bahari ya Hindi, mipaka yake haipaswi kwenda zaidi ya kilomita 22.2 kuingia baharini, ikifika 22.2 inakoma sehemu yote iliyobaki ni ya Watanzania wote sio ya mkoa fulani, sasa ukichukua hiyo sheria ya mikoa kuelekea huko baharini unaona kuwa gesi iliyopo Mtwara vijijini ni asilimia 14 tu ya gesi yote ambayo tumeigundua kwenye taifa hili, na ndugu zetu wa Lindi nao wana asilimia saba na Mkuranga wana asilimia moja tu.
Mpaka sasa gesi iliyogunduliwa asilimia 78 ni gesi ambayo haipo kwenye mipaka ya mkoa wa Mtwara, ipo kwenye mipaka ya Taifa letu wote kwa hiyo ni makosa kiutaalam na kisheria watu wa Mtwara mjini kujaribu kuwanyanganya Watanzania gesi yao, kwa sababu hii gesi sio ya watu wa Mtwara mjini mahali ambapo wamefanya maandamano, gesi nyingi imepatikana nje ya mipaka ya mkoa wa Mtwara.
Hili bomba, likishakamilika litasafirisha gesi ya futi za ujazo milioni 784 sasa gesi inayokuja huku ni ndogo nyingi itabaki huko huko, kwanza mtambo wa kusindika gesi asilia (LAG) ndio itakayochukua nyingi na yenye fedha nyingi zitapatikana.
Wale wanaoratibu yale maandamano wakae chini na kalamu wapige hesabu ya gesi kiasi gani kinachokuja Dar es Salaam na kiasi gani kinabaki Mtwara, waliofanya maandamano, hoja hapo haipo... hata kama wakitaka kujitenga, gesi waliyonayo wao ni asilimia 14 tu kutokana na gesi iliyogundulika mpaka sasa, gesi nyingi ipo kwenye kina kirefu cha maji ambayo ipo kwenye mipaka ya Tanzania na isitoshe cha muhimu sana wakati hii gesi, inatengenezeka mipaka ya bara la Afrika, Tanzania na Mtwara haikuwapo.
Hao wanaoratibu hayo maandamano naomba niwape fundisho, kwamba wakati gesi inatengenezeka kati ya miaka milioni 199.6 na milioni 23.03, hicho ndicho kipindi ambacho gesi hiyo imetengenezeka, mipaka haikuwapo kwa hiyo watu wa Mtwara mnaofanya maandamano hiyo gesi sio ya kwenu, kwa sababu wakati hiyo gesi inatengenezeka nyie hamkuwapo na hiyo mipaka haikuwapo.
Tusidanganywe, tusipotoshwe hiyo ni gesi ya Watanzania wote. Tusikubali kuvunjavunja taifa letu kwa sababu ya rasilimali zilizopo mikoani, wilayani au tarafa, kata na hata vijiji vyetu... Mungu awalaani wanaotaka kuvuruga amani na umoja wetu wa kitaifa, alisema Profesa Muhongo.