TANESCO kuanza kutumia nguzo za zege

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
588
1,698


Mramba-23July2015.jpg

Mkurugenzi wa Tanesco, Felchesmi Mramba

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lipo katika mchakato wa mwisho wa kuanzisha kampuni ya kutengeneza nguzo za umeme za zege, ikiwa ni mkakati wa uboreshaji huduma kwa wateja wake, kupunguza matumizi ya nguzo za miti na kudhibiti uharibifu wa miundombinu hiyo.

Akizungumza na NIPASHE jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Tanesco, Felchesmi Mramba (pichani), alisema kampuni hiyo ambayo itakuwa chini ya shirika hilo inatarajiwa kuanza kazi mwishoni mwa mwaka huu mchakato wa kuisajili kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) utakapo kamilika.

Alisema hatua ya shirika hilo kuanza kutumia nguzo za zege badala ya za miti ni moja ya mikakati ya shirika ilo kuhakikisha linatoa huduma bora na za uhakika kwa wateja wake kwani mara nyingi nguzo za miti zimekuwa hazidumu na kulazimika kubadilishwa mara kwa mara kutokana na uchakavu.

“Teknolojia inakuwa kila siku na kurahisisha huduma kwa wananchi na hata wakati mwingine kupunguza gharama, tutakapoanza kuzalisha nguzo za zege tutapunguza kero nyingi kwa wateja wetu kwani nguzo za miti huharibika haraka hasa kipindi cha mvua pamoja nyingine kuungua moto unapotokea,” alisema.
Mramba alisema kutumika kwa nguzo hizo za zege pia kutabadilisha mandhali ya miji na kuongeza kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania.

Kuhusu uboreshaji wa huduma ya umeme kwa jiji la Dar es Salaam, Mramba alisema ujenzi wa vituo vidogo vitano vya usambazaji na upozaji wa umeme unaendelea vizuri pamoja na changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika eneo la Mbagala na Vijibweni na kusababisha kazi hiyo kuchelewa kukamilika.

Alisema vituo hivyo vilitakiwa kuwa tayari mwezi ujao lakini kutokana na changamoto hizo sasa vitakamilika mwishoni mwa mwaka huu na kwamba kituo cha Kinyelezi na City Centre vinategemewa kukamilika Agosti, mwaka huu.

CHANZO: NIPASHE
 
Harufu ya upigaji pesa ileee .....

Ulijuaje mkuu?
Ndo nimeisikia sasa hivi unless kama kuna wataalamu wengine waje watuambie kama wenzetu huko nje wanafanyaga hiyo makitu.
Nnachojua ni kuwa wenzetu walioendelea hawajazi jazi manguzo barabarani isipokuwa wana lay wires underground.
Hii sijui imekaaje.
nasubiri kujifunza toka kwa wadau wengine.
 
Ulijuaje mkuu?
Ndo nimeisikia sasa hivi unless kama kuna wataalamu wengine waje watuambie kama wenzetu huko nje wanafanyaga hiyo makitu.
Nnachojua ni kuwa wenzetu walioendelea hawajazi jazi manguzo barabarani isipokuwa wana lay wires underground.
Hii sijui imekaaje.
nasubiri kujifunza toka kwa wadau wengine.


zilikuwepo,nakumbuka chole road ilikuwa na nguzo za zege[za taa za barabarani] chache zimesalia,nyingi zimegongwa na magari.
 
Wacha wabadilishe aise tuone sasa waganga wa jadi watabandika wapi vibao vyao..nilileta mada hapa kwanini tanesco inawaachia waganga kutangaza mabango yao..mod wakaifungia
 
Kwa nchi zilizo endelea ni kweli hawatumii nguzo kusambaza Umeme haswa maeneo ya mjin kwa nchi zetu za Africa bado sababu kubwa ni gharama za kutumia underground cable ni mara 3 ya gharama za kutumia nguzo Maeneo mengi nchini hayajapata Umeme kwa sasa ni Asilimia 40 tu wana access Umeme wenzetu mfano M are kabisa, Uingereza wanaongelea 98 plus access level Tunatumia pesa inayopatikana kupeleka umeme vijijin.
 
Back
Top Bottom