Tanesco kuandamana

Tanesco kuandamana

Wana jf kwa mujibu wa taarifa ya habari ITV wafanyakazi wa tanesco watangaza maandamano nchi nzima kupinga malipo ya DOWANS je ni uzalendo umefika

nimefurahishwa sana na uthubutu huu wa wafanyakazi wa tanesco ,, japokua mimi sio mfanyakazo wa tanesco, lakini siku ya maandamano, naahidi kua pamoja nao bega kwa bega,,
 
Hii ni janja yao, kimsingi serikali imegundua harakati ndizo zinazoupa upinzani nguvu, hivyo ili kupunguza nguvu ya upinzani kile ambacho kinataka kufanywa na upinzani kinapokwa ili upinzani utakapokuja kujifanya wanataka kufanya inakuwa ni kama marudio na hoja inakosa mashiko. Tanesco kuandamana ni changa la macho,
 
Sidhani kama serikali wanahusika. Hv umewasahau wafanyakazi wa Tanesco kwa upraisings za ukweli? Plz consult ur library, sasa hapa serikali ikae chonjo kumbuka umeme ni ishu bongo na ikiwa wafanyakazi wa umeme ndo wanagoma hapo pagumu. Tuombe kwa mungu jamani ya wenzetu tuyaone aljazeera tu! Ila sio ishu waandamane tu kwani kitu gani bunge limeshinda itakuwa wao! Haya tuone! Mwenye lake moyoni aseme!
 
Kama ni kweli basi ukombozi unanukia ktk hii THE FORGOTTEN COUNTRY! God Bless Tanzania!
 
uliza uambiwe. Ila tusifikie huko, we are smarter than that bandugu.
 
Hii ni janja yao, kimsingi serikali imegundua harakati ndizo zinazoupa upinzani nguvu, hivyo ili kupunguza nguvu ya upinzani kile ambacho kinataka kufanywa na upinzani kinapokwa ili upinzani utakapokuja kujifanya wanataka kufanya inakuwa ni kama marudio na hoja inakosa mashiko. Tanesco kuandamana ni changa la macho,

una akili? Kwan tanesco wote ni serikali? Kwa taarifa tanesco wapiganaji!
 
Hongera sana tuico tanesco huu ni wakati wa vyama vyote rafiki wa tuico kuunga mkono azimio hili na kuitisha maandamano haraka na kuonyesha nguvu za wafanyakazi
 
Wana jf kwa mujibu wa taarifa ya habari ITV wafanyakazi wa tanesco watangaza maandamano nchi nzima kupinga malipo ya DOWANS je ni uzalendo umefika

Mkubwa! Weka alama za nyakati twafadhali! Ndio uzalendo ume2fika na ndiyo maana tunasoma alama za nyakati1
 
Waangalie wasitupe mhemko, tukahemka km ilivyokuwa TUCTA then mnaahirisha kuandamana..! Tanesco wakifanikiwa kuandamana hata km 2 tu watakuwa wameamsha spirit flani hv ya uthubutu! U CAN DO IT TANESCO.....!
 
NITAKUWA PAMOJA NAO! Hakuna Malipo kwa kikundi cha wahuni. NEVER.
Na mikataba yote ya TANESCO iangaliwe upya, JK timiza ahadi yako ya tokea 2005 ya kupitia mikataba upya! Ukifanya hilo kwa dhati tutakusamehe!!?
 
Sidhani kama serikali wanahusika. Hv umewasahau wafanyakazi wa Tanesco kwa upraisings za ukweli? Plz consult ur library, sasa hapa serikali ikae chonjo kumbuka umeme ni ishu bongo na ikiwa wafanyakazi wa umeme ndo wanagoma hapo pagumu. Tuombe kwa mungu jamani ya wenzetu tuyaone aljazeera tu! Ila sio ishu waandamane tu kwani kitu gani bunge limeshinda itakuwa wao! Haya tuone! Mwenye lake moyoni aseme!

Big-up, maandamano siyo suluhisho, wanaweza kufanya hivyo kwa nia njema, lakini mataifa ya magharibi yanavyomezea mate matukio kama hayo ili malengo yao yatimie hasa ukizingatia kuwa tayari yana vibaraka wao katika nchi zetu. Tuombe mungu sana manake hisia mbaya zimeshapandikzwa miongozi mwa baadhi ya watu wetu , hivyo wanaweza kuunganishia humo ikawa nuksi
 
Hebu nieleze, Taaa nesi co anaandmana kupinga Dooo wan zi asilipwe au anaandamana kupinga taaa nesi co asimlipe dooo wan zi?, kuna jambo linahitaji clarification hapa; kumbuka kuwa mkataba wa awali ulikuwa kati ya tanesco na Dowans(hata kama ulishinikizwa na siasa), lakini mzogo umukuwa mkubwa zaidi bada ya siasa kuingilia na kufuta mkataba-si tanesco aliyevunja mkataba. Kwa hiyo aliyevunja mkattaba alipe gharama na mikataba yote aliyofanywa kisiasa ivunjwe ili isiendelee kuiumiza Tanesco.
 
Wana jf kwa mujibu wa taarifa ya habari ITV wafanyakazi wa tanesco watangaza maandamano nchi nzima kupinga malipo ya DOWANS je ni uzalendo umefika

Tanesco wazinguaji tu. Wanazuga kwakuwa wameona kila mtu anapinga, mbona walikaa kimya mda mrefu kama kweli inawauma kuwalipa dowans. Napata mashaka juu ya utashi wao.
 
Kwa bongo kuamini maandamano yoyote hadi niwaone barabarani vinginevyo tunadanganyana tu!
 
Nawaunga mkono wafanyakazi wa TANESCO kwa kutangaza maandamano nchi nzima dhidi ya malipo hewa ya DOWANS!

Tunakumbuka sana maandamano ya wafanyakazi hao mwaka 2002 kupinga serikali kuingizwa kwa kampuni ya kitaperi ya NET GROUP SOLUTION (Pty). Mh. Mkapa alisimama kidete ktk sakata hili na hatimaye matapeli hawa waliingia ubia na TANESCO. Walichofanya wahuni hawa kila mtu anakumbuka. Tuko nyuma yenu wafanyakazi wa TANESCO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Nami ingawa sio mfanyakazi wa Tanesco, lakini nitakua nao kama Muandamaji Mualikwa
 
Back
Top Bottom