jambotemuv
JF-Expert Member
- Feb 7, 2008
- 224
- 62
Matukio ya raia kufa kwa ajali za umeme wilayani Moshi kufuatia hitilafu za wazi katika miundombinu ambazo TANESCO walitaarifiwa mapema na zikapuuziwa sasa yamezidi. Hivi majuzi kafa baba mmoja huko Marangu Moshi (Goodhope Mshanga) alipojikwaa shambani mwake na kuangukia waya ushikiliao nguzo ardhini (stay wire) na kumbe ulishagusana na nyaya za moto juu baada ya tawi kubwa la mti kuziangukia nyaya. TANESCO Himo walitaarifiwa mara kadhaa lakini hawakufanya lolote. Marehemu Mshanga amekuwa mtu wa pili kufa kwa umeme kijijini Sembeti baada ya mtoto wa bwana Manyanga, na vifo vyote vikihusisha 'stay wire'.
Aidha zipo nguzo nyingi za zilizoliwa mchwa na kuangukia miti mashambani humu na taarifa zimetolewa lakini TANESCO hawajali. Waungwana tumlilie nani kwa hili???? TANESCO Moshi mwataka wafe wangapi ndo mjali???