TANESCO Kibaha badilikeni

TANESCO Kibaha badilikeni

FURY BORN

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2020
Posts
637
Reaction score
1,152
Merry Christmas wana jamvi,
Niende moja kwa moja kwenye mada Tanesco Kibaha ambayo ndo inawakilisha Tenesco mkoa wa pwani, imejaa ubabaishaji na kuendekeza rushwa. Nasema HILI kwa sababu moja.

Mkoa wa Pwani ni mojawapo ya mikoa ambayo inakuwa kwa kasi sana, lakini pia ni mojawapo ya mikoa ambayo imepitiwa na miradi mbalimbali iliyo chini ya shirika la umeme.

Maeneo nilioko mimi ni maeneo yaliyopitiwa na mradi wa nguzo za zege, mradi umekamilika kabisa, shida ni Tanesco kuaunganishia wateja umeme.

Hapa ni rushwa tupu na hii rushwa inaanza unapopeleka mchoro. Ukishafikisha mchoro wako wanaupokea na kukwambia nenda tutakupigia simu kukupangia suryeyor.

Lakini pindi unapotoka tu nje ya ofisi kuna mtu atakufuata na kukuliza bro nyumba yako iko eneo gani?

Kama unataka surveyor wa haraka chukua namba ya simu, ila kama hauna haraka nenda kasubiri, japo naamini utakaa sana.

Kwa udadisi wangu na kutaka kujiridhisha zaidi nikamwambia mhusika sawa nikimuitaji surveyor nje ya ofisi ni shilingi ngapi za kitanzania, bila wasiwasi akanijibu laki moja.

Na je nikishakupatia hilo laki moja ni nini kinafuata? Jibu Surveyor akisha survey utapatiwa control namba ambayo utaenda kulipa malipo halali ya Serikali kiasi cha shilingi laki tatu na ishirini.

Ukishalipia hiyo ya Serikali yule anayekuja kuunganisha umeme naye anatataka laki na nusu.
Na endapo sitokuwa na hiyo hela ina maana sitapata umeme?

Endapo utakuwa kichwa ngumu umeme utausikia na kuuona kwa jirani kwa sababu surveyors tuko wachache na bosi atatupangia kazi kulingana na watu walio mpatia hela, ndio maana na mimi nataka kutumia muda wangu nije nikufanyie survey.

Swali ni je ni mapato kiasi gani ambayo watumishi wa Tanesco Kibaha wanaikosesha Serikali kwa sababu ya kutaka rushwa ya laki moja?

Ukiachana na mimi nyumba kibao ambazo zimepitiwa na huo mradi hazina umeme na umeme upo, binafsi baada ya kukataa kutoa rushwa sijawahi muona surveyor tangu mwezi wa tisa mpaka leo hii.

Majirani zangu walioamua kutoa rushwa tayari wanao umeme. Mimi nimeapa sitotoa rushwa kwa kuwa ninayo solar yangu na pasi yangu ya mkaa ngoja wakae na umeme wao.

Kwa hiki kibarua changu kodi ninayolipa Serikalini ni kubwa mno, lakini pia katika zile billion ngapi kwa mwezi ambazo Serikali inatoa kwa ajili ya elimu bure huko nako mimi nimeipunguzia Serikali mzigo kwa kulipia gharama hizo moja kwa moja.

Tanesco Kibaha badilikeni la sivyo nimejipanga kurudi kivingine hasa wewe jamaa ambaye ndo unawapangia masurveyor kazi pamoja surveyors wako, nitakuja tena najua bado mnaitaji hii laki moja yangu, itaondoka nanyi.
 
Kibaha kila jambo ni shida,trafik wanapiga fine hata kama una fotokop ya kadi ya gari
 
Tafadhali tusaidie ni nani uliyewahi kumpatia hela au kumuona akipokea rushwa? Unaweza kutusaidia kwa kutupatia taarifa kamili au kufikosha TAKUKURU kwa siri ili kuchukuliwa hatua stahiki
 
Tanesco Kibaha kuna tatizo kubwa sana la kiutawala na utendaji mzima wa kazi zao za kila siku, mfano Kwa matias kuna tatizo la fuse kulipuka na kukata umeme kila mara kama sio kila siku mfano leo imelipuka tangu jana usiku saa 6 na wamekuja asubuhi wametoa fuse na kuondoka, inaelekea ofisi ile ina watu incompetent wanaoshindwa kujua na kutatua tatizo hilo ambalo kimsingi hata mwanafunzi wa DIT anaweza tatua

IMG_20210428_072904.jpg

IMG_20210428_072958.jpg
 
Hivi huyu meneja wa kibaha anaachwaje ofisini kwa kushindwa kuleta suluhisho kwa tatizo dogo tu la fuse hapa kwamatias? Tatizo hili limekuwa linatokea kila mara usiku na lilianza pale walipohamisha nguzo kupisha ujenzi/utanuzi wa barabara, bila kutaja matukio yote leo tena tumelala giza kwa uzembe wa mtu mmoja tu ambaye hana creactivity inayoenda na wakati , angalia kidude kilichomshinda ambacho hata mwanafunzi wa veta anaweza kukishughulikia
IMG_0019.jpg
IMG_0019.jpg
 
Naomba kujua huyo meneja wa kibaha bado yupo au alihamishwa? Nataka kwenda kufatilia umeme kwenye kiota changu
 
Hivi huyu meneja wa kibaha anaachwaje ofisini kwa kushindwa kuleta suluhisho kwa tatizo dogo tu la fuse hapa kwamatias? Tatizo hili limekuwa linatokea kila mara usiku na lilianza pale walipohamisha nguzo kupisha ujenzi/utanuzi wa barabara, bila kutaja matukio yote leo tena tumelala giza kwa uzembe wa mtu mmoja tu ambaye hana creactivity inayoenda na wakati , angalia kidude kilichomshinda ambacho hata mwanafunzi wa veta anaweza kukishughulikia
View attachment 1810939View attachment 1810939
Tumepokea taarifa kwa hatua zaidi tafadhali

Tupatie namba ya simu kwa ufatiliaji na mtejesho tafadhali
 
Haina sababu ya namba ya simu, mtoa taarifa kashatimiza wajibu wake, kawapa TANESCO hints za kuanzia uchunguzi, fatilieni mjiridhishe huyu mleta mada kashamaliza kazi yake
 
Tumeshapokea na kuanza kufatilia taarifa lakini namba ikipatikana inarahisisha hata kumfikia na kumuona mteja wetu.
 
Tanesco Kibaha kuna tatizo kubwa sana la kiutawala na utendaji mzima wa kazi zao za kila siku, mfano Kwa matias kuna tatizo la fuse kulipuka na kukata umeme kila mara kama sio kila siku mfano leo imelipuka tangu jana usiku saa 6 na wamekuja asubuhi wametoa fuse na kuondoka, inaelekea ofisi ile ina watu incompetent wanaoshindwa kujua na kutatua tatizo hilo ambalo kimsingi hata mwanafunzi wa DIT anaweza tatua

View attachment 1766210

View attachment 1766211
Ndugu mpendwa mteja wetu!

Tunashukuru sana kwa taarifa yako, Wataalamu wetu wamefika eneo husika kufanyia kazi taarifa zako ili kutatua tatizo,

Endelea kutupatia ushirikiano wako tafadhali.

TANESCO huduma Kwa Wateja
 
TANESCO mkoa wa pwani kwa ujumla ni wababaishaji, mimi nipo mkoa wa pwani kata ya vikindu kijiji cha picha ya ndege kitongoji cha kamegele huku wananchi tumejenga nyumba kufuru, lakini kitongoji hadi ninapoongea nyumba zinazowaka umeme hazifiki 20. Tanesco wababaishaji hatari, mimi mwenyewe walinitapeli 50,000 kuna surveyor mmoja anaitwa Omary yupo pale mkuranga, na kuna boss mmoja anahusika na mambo ya nguzo anaitwa swaleh gwara, yani nimewataja live live ili mjue watumishi wa Tanesco wanaihujumu serikali hii. Wanaikosesha nchi mapato kwa ajili ya tamaa za kupata pesa chafu. Hadi sasa kitongoji cha kamegele kipo gizani pamoja na majumba ya gharama yaliyojengwa hapa. What a shame.
 
Tumepokea taarifa tafadhali tusaidie namba yako ya simu uongozi ukusikilize zaidi
 
Tujaribu kuwa na akili kidogo jamani tatizo umeelezwa wewe bado unataka namba for what? Kuweni active na hamtaona mtu akilalamikia Tanesco
 
Sisi mtaa wa Mwambisi Kongowe Kibaha,tumewekewa laini ya Umeme na kulipia fedha kwa Control nno.ili kuunganishiwa umeme kwenye majumba,lakini mpaka leo hatujui kinachoendelea!
 
Back
Top Bottom