PSEUDOPODIA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2020
- 376
- 735
Habari wakuu, Mimi leo naomba nitoe kero yangu kwa ndugu zetu wa TANESCO huku Chanika. Katika mtaa wa kidugalo tumegawanywa kwa mashina, Sasa kutokana na baadhi ya mashina hatukumpa kura mwenyekiti wetu wa mtaa wakati wa uchaguzi wa ndani, hivyo wakati TANESCO wanaleta umeme huku wakapokea maagizo toka kwa mwenyekiti kwamba shina hili na hili sitaki wapate umeme.
Kuhusu huyu mwenyekiti sisi hatuna shida nae maana tunajua yeye ndo kirusi katika maendeleo ya mtaa wetu, Tatizo ni Tanesco kukubali kufuata maagizo hayo mwenyekiti.
Tunamwomba diwani kata ya Chanika, Mbunge, mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa, waziri wa nishati na madini au hata waziri mkuu maana tunajua yeye ni mfatiliaji mzuri wa keroe za wananchi na hata kama yupo bize kiasi gani yupo radhi kuacha shughuli zake na kuja kusikiliza kero za wananchi wakee. Tunaomba mje huku kututatulia kero yetu hii ilietuweze kwenda sambamba na kasi ya mama yetu Samia katika kuleta maendeleo ya nchi yetu.
Naamini litawafikia hili mjee mjionee ubaguzi wa waziwazi hukue kwetu Chanika kidugalo.