Tanesco imefilisika?

SonGod emo

Member
Apr 5, 2012
17
12
Hii hali sio shwari wiki iliopita kuna gazeti liliandika mgao wa umeme umeanza Tanzania bila ya taarifa yoyote kesho yake Tanesco walitangaza kupitia vyombo vya habari kwamba hizo taarifa ni za kizushi hakuna mgao wowote nchini ila ukweli ni kwamba mgao upo kama kawa leo hii kanda ya kaskazini kuna mitaa tumekaa zaidi ya saa kumi kwa siku halafu wanasema hakuna mgao.Tunaomba kuwe na ratiba maana watu wanateseka pasipo sababu.
Taaza za ukweli toka ndani vyanzo Tanesco wenyewe ukweli ni kwamba mitambo haina mafuta ya kuzalisha umeme alafu wanajitamba kulikoni Tanzania na uongozi wa ndiyoooooooo!!!!!!
 
Nani kakwambia kuwa Tanzania mgao utakuwa historia wakati bado tunatumia umeme wa maji tena kwa kutumia miundombinu ya enzi za mkoloni? Mgao upo na utaendelea kuwepo mpaka hapo tutakapopata viongozi thabiti watakaoona kuwa wizara ya Nishati na Madini si sehemu ya kuchezea kiduku
 
Back
Top Bottom