Tanesco Iliilipa Dowans Bilioni 1.4 kwa Makosa - CAG | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco Iliilipa Dowans Bilioni 1.4 kwa Makosa - CAG

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Apr 26, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Wanajamvi;

  Haya masuala hayawezi kamwe kwisha iwapo wahusika wanakenuliwa meno tu na JK na serikali yake. JK yuko tayari kila mara kuwaambia wananchi -- "Kuongezeka kwa gharama za umeme hakuepukiki" plus other nionsense , lakini kuwaajibisha wezi na mafisadi wahusika hawezi -- hutetemeka miguu. Sijui huwa anapewa mgao?  Kashfa mpya ya Ufisadi Tanesco:

  * CAG ADAI IMEILIPA DOWANS BILIONI MOJA ISIVYO HALALI

  Mwandishi Wetu

  SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), limeingia katika kashfa nyingine ya ufisadi baada ya kubainika kuwa limeilipa Kampuni ya kufua umeme ya Dowans dola za Marekani 1.2 milioni ikiwa ni gharama ya kusafirisha mitambo ya kampuni hiyo kuja nchini kwa ndege badala ya dola 120,000.

  Matumizi hayo ya ziada yanayokadiriwa kufikia Sh1.4 bilioni za Tanzania yanaelezwa kwamba yaliingizwa katika akaunti ya Dowans kimakosa.

  Hata hivyo, mpaka sasa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), amesema Tanesco imeshindwa kumpelekea ripoti ya matumizi ya fedha hizo alizoziita kuwa ni ufisadi.

  Mbali na hivyo CAG amelitaka shirika hilo limpelekee mchanganuo wa matumizi ya dola za Marekani 4,865,000 sawa na Sh6.8 bilioni.

  Jana, alipotakiwa kufafanua kuhusu ripoti hiyo, CAG Ludovic Utoh alisema: "Nashukuru kwa kunipigia, lakini nyie si mnazo ripoti hizo, mnaweza mkasoma na kuendelea kuripoti."

  Kwa mujibu wa gazeti la The East African, toleo la Aprili 25, mwaka huu, ripoti ya CAG iliyoishia Juni 30, 2010 inaonyesha kuwa Tanesco ilifanya malipo hayo kupitia akaunti ya gharama za mikutano.

  Taarifa hiyo imeonyesha kuwa Tanesco ilishindwa kutoa maelezo kuhusu malipo hayo kwa ajili ya kukodisha ndege maalumu ya kusafirishia mitambo hiyo. Pia inaonyesha kuwa kiasi cha Sh13,000,000 ziliripotiwa kimakosa kama Sh1,300,000,000 kwenye kifungu cha matumizi ya vikao na pia kiasi cha Sh11.0 bilioni kinachohusu malipo kupitia barua ya mkopo (letter of credit) na kuingizwa katika akaunti ya makusanyo ya shirika kupitia benki ya NBC.
  CAG pia alibaini kuingizwa mara mbili kwa Sh101 milioni katika akaunti ya mitambo ya Tanesco kinyume na taratibu.

  CAG alisema kuwa ndani ya Tanesco hakufanyiki usuluhishi wa mapato yatokanayo na mauzo katika matawi yake kukiwemo pia jumla ya Sh103,000,000 za masurufu ambazo hazijarejeshwa. Pia umeme unaozalishwa na ule unaouzwa unaonyesha kwamba shirika hilo linapata hasara kutokana na sababu za kiufundi.

  Ripoti hiyo inasema, Tanesco ilionyesha hasara za uniti 1,188 KwH'm kutoka katika uniti 4,831 KwH'm inazozalisha ikionyesha kwamba kuna hasara katika mapato. Hasara hizo zinachangiwa na kuwepo kwa wateja wasio waaminifu, bili za uongo na uunganishaji haramu wa umeme.

  Imeeleza kwamba hata wateja waliokatiwa umeme, wanaendelea kutumia huduma hiyo kama kawaida licha ya kudaiwa wastani wa dola za Marekani 65,000.CAG, Utouh alikaririwa akisema manunuzi katika shirika la Tanesco yalirekodiwa kimakosa na kwa udanganyifu.

  Utouh alisema wakati wa ukaguzi, iligundulika kwamba Tanesco, hawakuwa wakifanya ‘reconciliation' (upatanisho) ya mwezi kati ya mauzo na mapato.Kwa mujibu wa CAG, kuna hasara katika idara za uzalishaji na usambazaji wa umeme kwenda wateja.

  " Kuna mapendekezo niliyoyatoa yanayotakiwa kuchukuliwa hatua na Serikali, Bunge, Kamati ya Hesabu za Serikali, Bodi ya Wakurugenzi na maofisa watendaji wakuu kupitia ripoti ya fedha iliyoishia Juni 30,2009," ilisema ripoti hiyo.

  Katika ripoti hiyo, CAG alisema katika ripoti ya mwaka uliopita ya ukaguzi katika mamlaka za umma na bodi nyingine kuna mapendekezo 15 yaliyotolewa kwa utekelezaji: "Lakini hadi sasa mapendekezo hayo hayajatekelezwa kikamilifu."

  Alisema mapendekezo hayo ambayo hayajatekezwa yanahitaji ufumbuzi wa Serikali ili kuyawezesha mashirika mengine ya umma kufanya vizuri.

  Badra Masoud, Meneja mahusiano wa Tanesco hakuweza kupatikana jana kuzungumzia suala hiyo baada ya simu yake kuita muda wote bila kupokelewa huku simu ya Mkurugenzi wa Tanesco William Mhando ikiwa haipatikani.

  Chanzo: Mwananchi.
   
 2. k

  kakini Senior Member

  #2
  Apr 26, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kama ingekuwa mimi ndo rais ningewayonga wooote haoo
   
 3. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Bila kuiga mfano wa China wa kuwapiga risasi mafisadi hadharani bado ufisadi utaendelea kutawala Tanzania huku viongozi wenyewe wakiwa vinara.BIla serikali mpya,watu wapya kuongoza nchi hakuna mabadiliko.JK alisema atawataja wauza unga hadi leo kimya,akaahidi kuwashughulikia mafisadi hadi leo kimya,ipo haja ya watanzania kuamka kudai haki.
   
 4. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wanaochomwa moto ni vibaka tu na wezi wa kuku? Vipi hawa wezi wa mamilioni tena ya watu wengi? Nafikiri wananchi tufikirie vilevile kujichukulia hatua mikononi mwetu kwa hawa watu wanaotuibia mali zetu za umma. Hii haiwezi kuvumilika hata kidogo.
   
 5. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #5
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  hiyo ni tanesco tu !viongozi hawa kama jk, ccm na serikali yake.mambo yako hivi au hata zaidi karibu kwa taasisi na mshirika yote ya umma.ccm chama cha mafisadi au chukua chako mapema
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,786
  Trophy Points: 280
  Kashfa mpya ya Ufisadi Tanesco, Tuesday, 26 April 2011 10:14

  [​IMG]
  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovic Utoh

  CAG ADAI IMEILIPA DOWANS BILIONI MOJA ISIVYO HALALI
  Mwandishi Wetu
  Mwananchi

  SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), limeingia katika kashfa nyingine ya ufisadi baada ya kubainika kuwa limeilipa Kampuni ya kufua umeme ya Dowans dola za Marekani 1.2 milioni ikiwa ni gharama ya kusafirisha mitambo ya kampuni hiyo kuja nchini kwa ndege badala ya dola 120,000.

  Matumizi hayo ya ziada yanayokadiriwa kufikia Sh1.4 bilioni za Tanzania yanaelezwa kwamba yaliingizwa katika akaunti ya Dowans kimakosa.
  Hata hivyo, mpaka sasa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), amesema Tanesco imeshindwa kumpelekea ripoti ya matumizi ya fedha hizo alizoziita kuwa ni ufisadi.
  Mbali na hivyo CAG amelitaka shirika hilo limpelekee mchanganuo wa matumizi ya dola za Marekani 4,865,000 sawa na Sh6.8 bilioni.
  Jana, alipotakiwa kufafanua kuhusu ripoti hiyo, CAG Ludovic Utoh alisema: "Nashukuru kwa kunipigia, lakini nyie si mnazo ripoti hizo, mnaweza mkasoma na kuendelea kuripoti."

  Kwa mujibu wa gazeti la The East African, toleo la Aprili 25, mwaka huu, ripoti ya CAG iliyoishia Juni 30, 2010 inaonyesha kuwa Tanesco ilifanya malipo hayo kupitia akaunti ya gharama za mikutano.
  Taarifa hiyo imeonyesha kuwa Tanesco ilishindwa kutoa maelezo kuhusu malipo hayo kwa ajili ya kukodisha ndege maalumu ya kusafirishia mitambo hiyo. Pia inaonyesha kuwa kiasi cha Sh13,000,000 ziliripotiwa kimakosa kama Sh1,300,000,000 kwenye kifungu cha matumizi ya vikao na pia kiasi cha Sh11.0 bilioni kinachohusu malipo kupitia barua ya mkopo (letter of credit) na kuingizwa katika akaunti ya makusanyo ya shirika kupitia benki ya NBC.
  CAG pia alibaini kuingizwa mara mbili kwa Sh101 milioni katika akaunti ya mitambo ya Tanesco kinyume na taratibu.

  CAG alisema kuwa ndani ya Tanesco hakufanyiki usuluhishi wa mapato yatokanayo na mauzo katika matawi yake kukiwemo pia jumla ya Sh103,000,000 za masurufu ambazo hazijarejeshwa. Pia umeme unaozalishwa na ule unaouzwa unaonyesha kwamba shirika hilo linapata hasara kutokana na sababu za kiufundi.
  Ripoti hiyo inasema, Tanesco ilionyesha hasara za uniti 1,188 KwH'm kutoka katika uniti 4,831 KwH'm inazozalisha ikionyesha kwamba kuna hasara katika mapato. Hasara hizo zinachangiwa na kuwepo kwa wateja wasio waaminifu, bili za uongo na uunganishaji haramu wa umeme.

  Imeeleza kwamba hata wateja waliokatiwa umeme, wanaendelea kutumia huduma hiyo kama kawaida licha ya kudaiwa wastani wa dola za Marekani 65,000.CAG, Utouh alikaririwa akisema manunuzi katika shirika la Tanesco yalirekodiwa kimakosa na kwa udanganyifu.

  Utouh alisema wakati wa ukaguzi, iligundulika kwamba Tanesco, hawakuwa wakifanya ‘reconciliation' (upatanisho) ya mwezi kati ya mauzo na mapato.Kwa mujibu wa CAG, kuna hasara katika idara za uzalishaji na usambazaji wa umeme kwenda wateja.

  " Kuna mapendekezo niliyoyatoa yanayotakiwa kuchukuliwa hatua na Serikali, Bunge, Kamati ya Hesabu za Serikali, Bodi ya Wakurugenzi na maofisa watendaji wakuu kupitia ripoti ya fedha iliyoishia Juni 30,2009," ilisema ripoti hiyo.

  Katika ripoti hiyo, CAG alisema katika ripoti ya mwaka uliopita ya ukaguzi katika mamlaka za umma na bodi nyingine kuna mapendekezo 15 yaliyotolewa kwa utekelezaji: "Lakini hadi sasa mapendekezo hayo hayajatekelezwa kikamilifu."
  Alisema mapendekezo hayo ambayo hayajatekezwa yanahitaji ufumbuzi wa Serikali ili kuyawezesha mashirika mengine ya umma kufanya vizuri.

  Badra Masoud, Meneja mahusiano wa Tanesco hakuweza kupatikana jana kuzungumzia suala hiyo baada ya simu yake kuita muda wote bila kupokelewa huku simu ya Mkurugenzi wa Tanesco William Mhando ikiwa haipatikani.
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Haya bwana,

  Hivi hawa mafisadi wataguswa vipi wakati wanazidi kujichotea mikwanja. Mimi nilidhani mianya ya kuwapatia cheap money ilishazibwa kumbe ndo imefunguliwa!!!!

  Tufwile banyambalaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!
   
 8. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Duu shirika letu linaelekea kufa!!
   
 9. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  wataalamu wa kukwapua wanatonya kuwa wajanja wamechota mkwanja.

  Tanesko imegeuzwa bangusilo tu.
   
Loading...