Tanesco igeni mfano wa oryx katika kutunza mazingira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco igeni mfano wa oryx katika kutunza mazingira

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Njowepo, Dec 11, 2011.

 1. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Gharama ya gesi, mitungi kushuka
  Na Mwandishi wetu
  30th November 2011

  Mitungi ya gesi ya Oryx

  Kampuni ya kuuza na kusanbaza Gesi ya Oryx gass inatarajia kupunguza gharama za gesi na mitungi ya gesi kuanzia Desemba.

  Hayo yakisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Hamis Ramadhan, wakati akiongea na waandishi wa habari kwa lengo la kuielemesha jamii umuhimu na faida za kutumia nishati ya gesi.

  “Mpaka tarehe 10 Disemba tutakuwa tumepunguza bei za gesi na mitungi yake kwa nchi nzima na kuwawezesha wananchi kutumia gesi kama nishati mbadala itakayochangia kupunguza ukataji wa miti na misitu unaosababisha uharibifu wa mazingira, ” alisema.

  Hata hivyo, alisema kuwa matumizi ya gesi yameongezeka kutoka tani 300 mwaka 2006 hadi tani 2000 mwaka huu, na gharama za ununuzi wa gesi kutoka nje ya nchi zimeongezeka kutokana na kushuka kwa Shilingi.

  Meneja Bidhaa wa kampuni hiyo, Mafudhi Maulid, alisema pia watatoa mafunzo maalum ya matumiza ya gesi yatakayotokewa kuanzia Desemba lwa njia ya televisheni, redio na magazeti.

  Pia alitoa ombi kwa wananchi kutoa taarifa pindi watakapobaini muuzaji wa gesi anayeuza kwa bei ya juu tofauti na ile watakayoipanga wao watatoa adhabu kwa yeyote atakaye bainika kulingana na makubaliano yao kibiashara katika uuzaji wa gesi.
  CHANZO: NIPASHE
  MY TAKE
  Ukiongeza bei ya umeme watu watahamia kwenye kuni na mkaa na ukipunguza iyo bei ni kunyume chake na ndicho ambacho Oryx wanataka kukifanya.Home mtungi wa 50,000 natumia kwa mwezi so ikipungua mambo ya kuchnganya gesi na mkaa kwenye kupikia yatapungua.Si unajua mandondo lazima uanzie kwenye mkaa then baadae kwenye gesi
   
Loading...