Tanesco huu ni urasimu na wizi mtupuu!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco huu ni urasimu na wizi mtupuu!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Igangilonga, Jul 9, 2011.

 1. I

  Igangilonga Senior Member

  #1
  Jul 9, 2011
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 121
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wadau naomba nililete hili kwenu ili tushauriane, mimi kiukweli linanikwaza mnooo jinsi wizi huu wa kimachomacho tunaofanyiwa watanzania bila wenyewe kujijua wala kufikiri......

  Mwananchi akitaka kuweka mita ya LUKU kwake analipia zaidi ya laki 450 na bado mita inabakia kuwa ya Tanesco. Mwananchi akitaka kuvuta umeme kwake anatakiwa alipie nguzo moja sh. milioni 1, kwahiyo kama utatakiwa kuvuta nguzo tatu utalipa milioni 3 n.k. Wakati huo huo, mwananchi mwingine jirani na huyo aliyelipa 3 milion akitaka kuvuta umeme anafungiwa kutoka katika zile nguzo alizolipia mwenzie (manake hapo zinakuwa tayari ni za Tanesco) na anatozwa hela fulani, je sio kwamba wanamuonea yule alievuta mwanzo? Je hatakiwi na yeye kuwa compensated some amount kutoka kwa wale ambao watavuta kutoka katika nguzo alizoshalipia yeye mamilioni? Badala yake hela ya wateja wanaofuata inaliwa na Tanesco as if zile nguzo waliziweka wao bure katika kutoa huduma kwa jamii kumbe walimuuzia mwananchi wa kwanza kuvuta katika eneo hilo........mimi sielewi jamani huu utaratibu wao.......KAMA KUNA ANAEJUA WANAFANYAJE AU KAMA KUNA MTU WA TANESCO NAOMBA ANITOE DUKUDUKU LANGU HILI!!
   
 2. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,098
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Huu ni wizi uliohalalishwa na Serikali iliyoko madarakani, ambayo kimsingi ndio baba wa shirika hili.

  Mimi nliomba kumtenganishia Mita ya Luku Mpangaji wangu mmoja maeneo ya Mbezi Juu ambayo kuna wapangaji wengine wawili pia nikaambiwa eti mpaka wakiwa na Route ya kuja maeneo ya huko kwangu,

  Yaani eti nisubiri mpaka mitaa ya kwetu akitoeka mtu mwengine mwenye shida ya TANESCO ndio waniunganishe nae, kifupi nikae naomba mungu jirani zangu nao wapate shida kwenye mita zao ndio tuwe wengi kisha waje.

  Hii kadhia ukijumlisha na MGAO ndio chuki yangu juu ya shirika hili inapozidi kuongezeka kila kukicha. nafikiri wana laana ya zile rangi wanazozitumia
   
 3. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Utaratibu ni kwamba, gharama za kuunganishiwa umeme mfano kulipia nguzo inatakiwa wateja wagawane gharama! Na kama kuna mtu akitokea kulipia nguzo mwanzoni, basi wateja watakaofuata itawalazimu kumrudishia ile pesa mwenye kulipia kwanza. Hivyo ndivyo navyojua mimi hapa. Lakini, kutokana na mfumo mbovu wa shirika la letu la umeme, na watu wengi kutoelewa haki zao ndani ya shirika hili wakiwa kama wateja basi shirika linajiendeshea litakavyo.

  Tatizo kubwa hapa ni watu wanaounganisha(wafanyakazi) na wanaounganishiwa(wateja)! Wafanyakazi wengi wanapenda ufisadi, utakuta nguzo nyingi zilizopo mtaani ni za dili, wafanyakazi hao hao wakiwemo Wakuu wa vikosi ( Maintanance Engineers which actually are not Engineers) wanashirikiana na vishoke kufanya hiyo mipango na kujipatia utajiri wa haraka haraka. Wateja nao wameshajijengea mazoea bila kutoa kidogo hupati huduma ndo matokeo yake tatizo linakuwa siku hadi siku.
   
 4. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,757
  Trophy Points: 280
  Ha wala msiseme tnesc ni wanyang'anyi,tena wezi wa wa waziwaz hata bili zao wizi tu,umeme unakatika 24/7 af bili inakuja sawa na ya umeme ukiwa fulltime, ukipata chance unachokoroa mita kufidia upupu wao! Shenz type
   
 5. I

  Igangilonga Senior Member

  #5
  Jul 10, 2011
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 121
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  nakubaliana nanyi, ni watu wengi hawajui kuhusu hili...... sasa tufanyaje ili wananchi wajue na pia Tanesco wajue kuwa tupo wachache tunaojua uchafu wao huu? Kuna haja ya kuliweka hili wazi (public) kabisaaa...... mimi bado nalifanyia kazi nikipata uthibitisho ntawalipua washenzi hawa, hata ktk barua za maoni tu katka magazeti
   
 6. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  hatuwezi kuendelea kwa mifumo hii ya kuliwa hela live!
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Nilikuwa sielewi kwa nini watu wanakuwa rebels, terrorist, Snippers yaani kwa yanayotokea sasa hivi kwenye nchi yetu ni possible kabisa tutaanza zalisha kizazi cha hao niliowataja hapo juu. Yaani ni unyang'anyi unaofanyika mchana kweupeeeeee
   
Loading...