TANESCO, Geita, Uranium, Rushwa, Urais - Tanzania Twahitaji mhimili wa nne wa utawala!

puza46b

Member
Nov 3, 2010
91
261
Wanajamii naombeni ruhusa kutoa hii hoja ya ni kwanini Tanzania yahitaji muhimili wa nne wa serikali, faida yake na ni jinsi gani uundwe. Kwa sasa tanzania ina tume ya katiba, Kuna uwezekano mkubwa hii katiba ndiyo ikawa mwongozo mkuu wa nchi yetu kwa miaka mingi ijayo. Hivyo ni muhimu tufikirie mbali kujaribu kutatua matatizo ya kiutawala yanayoweza tokea hapo baadaye na tupunguze hivi viini macho vinavyoendelea bungeni.

Kwanza kabisa nitaanza kwa kuonyesha mapungufu ya mfumo uliopo sasa yaani Serikali ikiongozawa na raisi, Bunge na Mahakama.

Serikali (Rais na baraza lake),

  • Rushwa-Wote twajua maraisi wengi africa ni wala rushwa hivyo maslahi ya mwananchi wa kawaida hayalindwi.
  • Siasa mbele - Rais ni mwanasiasa.. demokrasia na uchumi ukikuwa tunaweza kuwa na matatizo ya kisiasa kama ya marekani ambapo raisi anapoteza miaka miwili ya mwisho ya term ya kwanza katika kampeni. Pia kampeni ni gharama na wale watakaolipia gharama ndo watakao endesha inchi.
  • Uwajibikaji -- Rais ana nguvu kubwa sana na uwajibikaji ni mdongo. Bado nasubiri kuangalia ni wanasiasa wangapi wataenda jela kwa madudu yanayoendelea.
  • Taaluma - mawaziri wengi wamekuwa wakichaguliwa kisiasa na unakuta waziri asiyejua chochote kuhusu kilimo akitoa maamuzi nyeti yahusuyo 80% ya uchumi wa taifa na uwamuzi wake ni wa mwisho. Na bado twashanga ni kwanini tanzania bado ni masikini.

Bunge.

  • Sababu zilizotajwa hapo juu zaweza wekwa hapa pia. Hii kashfa ya tanesco haitakuwa ya mwisho hivyo lazima bunge nalo likumbushwe pale linapoyumba na lisiwe na sauti ya mwisho bila kuangaliwa mara mbili.
  • kuna wakati bunge halitaweza fanya kazi kwa sababu ya kushindwa kufikia makubaliano kwa sababu za kisiasa. Mfano mzuri ni kilichoendelea Arusha baada ya uchaguzi wa madiwani. Kuna nchi zimekaa hadi mwaka bila kuwa na functioning goverment kwa sababu ya ubishi na chuki za kisiasa mfano Iraq, Greece na pia hoja nyingi zikwamazo kwenye senate marekani ni kisiasa zaidi. Hii hali inaweza tokea tanzania miaka ijayo ambapo wanasiasa wanakomoana badala ya kuweka maslahi ya wananchi mbele.
  • Ingawaje lobbying bado haijakuwa tanzania, kuna uwezekano mkubwa sana wale wenye uwezo wa kugharamia loby ndiyo matakwa yao yatapita bungeni. hili swala la lobbying likatazwe kwenye katiba yetu mpya hata kama hatuna muhimili wa nne wa utawala.
  • Wanasheria na siasa - bunge ni sehemu ya kutunga sheria ndiyo sababu wanasiasa wengi wanatoka kwenye fani ya sheria. tatizo ni kwamba maamuzi mengine yanahitaji kuangaliwa kisayansi zaidi kuliko kisheria na hapo nchi nyingi duniani zinadorora.


Mahakama

  • Rushwa - Ingawaje kuna mahakimu ambao wana utu na wanajali maslahi ya taifa na haki kwa ujumla, mahakimu bado ni binadamu pia itachukuwa miaka mingi kuwa na proffesionalism tanzania.
  • Siasa na uchaguaji wa majaji wakuu - kwa sababu jopo la majaji wa mahakama kuu wanateuliwa na rais, kuna uwezekano mkubwa wa kurudishiana fadhila. Mfano mkuu angalia tena marekani mahali ambapo majaji wanatoa maamuzi kulingana na mawazo ya kisiasa (na pia maamuzi yao ni sambamba kwa wale waliochaguliwa na raisi kutoka chama kimoja)

Sababu nyingine nyingi zaweza wekwa hapa ila muda sina na sina nia ya kuandika thesis bali nataka wanajamii tuangalie kwa undani ni nini cha kulilinda taifa letu na hidhi zambi za wanasiasa na wakati huo huo nchi iendelee.

Kwa sababu zilizotajwa hapo juu ndo maana naona kuna haja ya kuwa na muhimili wa nne wa utawala. Huu unaweza jengwa kwa kutumia wataalamu katika fani mbali mbali. kazi yao ni kuangalia maamuzi ya serikali na bunge kuhakikisha yanakidhi matakwa yafuatayo.
· maendeleo - Mfano mzuri ni austerity measure zinazoendelea ulaya ingwaje tatizo kuu la uchumi lilianzia bank. Hapo inatakiwa hao jopo la uchumi linalosimamia maamuzi ya kiserikali linaweza kuliangalia hilo na kutoa kura ya veto kama hazichangii kuokoa nchi na maisha ya mwanachi wa kawaida.
· Kisayansi - mfano sheria ya kulinda mazingira tanzania inayohusu makampuni yatakayochimba mafuta na yanayotoa madini kama ya uranium. Kuanzia land reclamation kwenye mining pit mpaka malipo ya maafa kwenye nchi/ jamii yoyote itakayoathiriwa na uchimbaji wa gesi na mafuta. Wanasayansi wanaweza waka veto sehemu inayohusika na jinsi ya kulinda au kurudisha mazingira na wana ustawi wa jamii waka veto kama hawakubaliani na maslahi ya jamii. Pia maamuzi yahusuyo nishati, afya, technologia na kadhalika yaweza kuhakikiwa vizuri.
· Hali halisi - maamuzi mengi yanatakiwa yaendane na hali halisi iliyopo nchini na eneo litakalo athiriwa. kwa mfano wazo la kumbunguza foleni kwa kuruhusu magari yapite upande mwingine wakasahau yatakutana mbele.
· Sababu nyingine ni vyote vilivyo opposite na mabaya ya miundo mitatu pekee.

Muundo wa huo muhimili wa nne unaweza patikana ukizingatia mambo yafuatayo;

  • Kuwe na majopo tofauti yanayoundwa na wanakamati watano (even number kupunguza deadlock)
  • majopo yanayoweza undwa ni kwa mfano,
    • Madaktari- walikosoe bunge kwenye mambo ya afya.
    • Wahandisi - wahakiki maamuzi ya miundo mbinu (mfano rapid transit system dar na ujenzi wa kigamboni wakati mikoa mingine ipo nyuma).
    • Wasomi wa kilimo wahakiki maamuzi yatakayo wagusa wakulima.
    • Wachumi - miaka 50 bado tu masikini tunahitaji kila mkono wa kutuokoa katika hili janga.
    • Architects and planers - hizi foleni zibaki dar hakuna sababu ya kuzipeleka tanzania nzima, hivyo basi tuwe na wataalamu watakao kosoa serikali. nakadhalika....
  • Wanajopo wateuliwe (nominated) na wanachama (practicing members) wa professional yao mfano wanachama wa ERB, MAT. masharti ya kuteua ni ujuzi na uzoefu walio nao kwenye fani zao.
  • Kusiwe na kupiga kampeni kwani kama mtu ni mjuzi katika fani utafahamika.
  • Wateuliwe kila miaka miwili na nusu na uchaguzi wao uwe mwaka mmoja kabla ya kuteua serikali na bunge. hii kuhakikisha kuna plan B pale matokeo yakitoa 50/50
  • pale kunapotokea deadlock ya kisiasa uamuzi wao uwe wa mwisho. hii itaondoa upuuzi bungeni.
  • Jopo liwe na uwezo wa kutengua uamuzi wa raisi (nadhani mahakama in nguvu hiyo pia ila yenyewe inaangalia kisheria tu) pale yanaposhindwa kufikia matakwa ya kimaendelea, kisayansi na kijamii
  • na kama serikali ikisimamishwa hapo baadaye (mfano raisi amekutwa na hatia au hakuna makubaliano bungeni ya nani awe waziri mkuu (sina uhakika ila nadhani bunge la tanzania linatakiwa kumpitisha waziri mkuu) ) kila mwanajopo amteue mmoja wao (asijiteue mwenyewe) na yule apataye kura nyingi aendeshe wizara inayoshughulikia fani yao mpaka pale hali ya kisiasa inaposuluhishwa. hapa pia kampeni hairuhusiwi.
  • Wanajopo watawajibishwa na bodi ya fani yao kama kutakuwa na proffessional missconducts.
  • Wanajopo hawatashauri serikali katika maswala ya mishahara kwa fani yao na hawana usemi katika hilo. isipokuwa wanaweza angalia mishahara wabunge wanayojipangia na kuipiga veto endapo hailingani na hali halisi ya taifa (wanauchumi watasimamia hili).
  • Sheria zote za conflict of interest zitachukua mkondo pale mwanajopo anaposhindwa kujitoa kwenye maamuzi yanayo ingiliana na biashara zake.
Kwa kweli naweza andika kurasa mia lakini siyo nia yangu kuwachosha.
Mnakaribishwa mchangie hii hoja, naombeni muweke siasa pembeni kwani swala la katiba ni kubwa kuliko hizi kelele za kisiasa. Vitukuu vyetu vitatuangalia na kutuhukumu kama tutaendlea kuwa na upeo mfupi. kama kuna mapungufu katika hoja yangu au kutoka kwa mchangia hoja toa wazo la jinsi ya kurekebisha badala ya kumshambulia mchangia hoja.

Kuna uwezekano mkubwa sitajibu maswali yatakayo letwa kwangu kwani niko bize sana. Isipokuwa nitasoma na nitajitahidi kujibu kadri niwezavyo ila kama nilivyosema hapo juu changia hoja.

Mungu Ibariki Tanzania.

Puza!
 
Back
Top Bottom