TANESCO Arusha wagoma, Umeme wakatika masaa 24

TANESCO Arusha wagoma, Umeme wakatika masaa 24

Mwana Kwetu

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2011
Posts
652
Reaction score
607
Hii imebainika baada ya umeme kukatika kwa masaa Zaidi ya 24 kwenye maeneo mengi ya mji wa Arusha IKIWEPO KATA NZIMA YA KIMANDOLU maeneo yote ya Kijenge, Themi na maeneo mengi ya Njiro na mjini kati. Jana Jumapili umeme ulikatika katika maeneo haya kuanzia saa 1 asubuhi na hadi ninapoandika habari hii bado umeme haujarudi na hakuna taarifa zozote kuelezea tatizo ni kitu gani. Kukatika kwa umeme kwa masaa zaidi ya 24 bila taarifa ni tukio ambalo halijawahi tokea katika historia ya mgao wa umeme tangu kuaniashwa kwa mji wa Arusha.

Hali hii inayodhihirisha wazi ni kitendo cha makusudi cha hujuma kinachofanywa dhidi ya Meneja wa mkoa kutokana na kutoridhishwa mambo kadha wa kadha.

Mgomo baridi huu wa wafanyakai wa TANESCO Arusha umeanza tangu mwezi wa February 2015. Hali hii imesababisha umeme kupatika kwa shida sana na mara nyingi unakatika kuanzia masaa 6 na kuendelea.

Kwa niaba ya waathirika namwomba Mkurugeni wa TANESCO ndg Mramba aungalie upya uongozi wa meneja wa TANESCO Arusha kwani hawa watu wamekuwa wakitoa majibu mepesi mno bila kujali athari ambazo watumiaji wa umeme wamepata ikiwa ni pamoja Vitu kuoza na biashara nyingi kupata hasara. Kuna uzembe wa hali ya juu unaotakiwa kushughulikiwa dhidi ya uongozi wa TANESCO Arusha ili hali ya upatikanaji umeme stable iweze kutengamaa.
Hasara hii inakuwa kubwa zaidi pale ambapo watumiaji wa LUKU wataendelea kupigwa kodi kubwa "base tax" bila kujali umeme ulikatika au la.
 
Aisee kama ni mateso tumepata makubwa, mimi niko Maeneo ya KIMANDOLU na ni kweli umeme ulikatika jana mida ya saa 1 asubuhi na hadi naondoka kwenda job umeme haupo. Huu umeme umekatika mfululizo bila kurudi hata saa 1. Hii inatakuwaje matatizo ya staff wa institution na wakuu wao yanaathiri watu wasio husika kwa kiasi kikubwa namna hiyo. Hapa tatizo kama ni Meneja si atolewe tu kuliko kuendele kuwataabisha innocents
 
F. Mramba tunaomba usimwangalie mtu usoni hapa tunateseka, tunapata hasara kwa sababu ya mtu mmoja aliyeshindwa kusimama kwenye nafasi yake sawasawa
 
F. Mramba tunaomba usimwangalie mtu usoni hapa tunateseka, tunapata hasara kwa sababu ya mtu mmoja aliyeshindwa kusimama kwenye nafasi yake sawasawa

Pole mkuu hii nchi inadidimizwa na viongozi wasanii na wabinafsi
 
Tangu jana maeneo mengi Arusha hayana umeme na hili tatizo limeanza a month ago
 
TANESCO ARUSHA watueleze kama usambazaji na usimamizi wa umeme umewashinda ili turudishe Net group solutions. Tunakumbuka Net Group Solutions walipokuwepo umeme haukukatika hadi walipoondoka tukarudi kwenye umeme wa kiswahili wa kukatika katika
 
Nafikir huu mgao ni kanda ya kaskzin, coz hata Mosh jana kulikua hakuna umeme had saa tano unusu usiku na umekatika saa 12 asubuh leo.
Nafikir TANESCO ni kati ya mashirika ambayo hayajapiga hatua yoyote toka 2005 na linazid kuleta hasara kwa mwananch na serikal kwa ujumla.
Wanasema hatua waliyopiga ni kusambaza umeme vijijin lakin hiyo ni ujinga kutumia umeme wa kuwashia taa tu na bili ni kubwa wakat wenzetu maana ya kuwa na umeme ni kuondokana na kutumia mkaa na kuanza kutumia vitu vya vinavyotumia umeme mfano kupikia jiko la umeme lakin huku ukitumia jiko la umeme utajikuta unatumia sh 50000 kwa mwez na ukiongezea na kupiga pasi ndo bas tena
 
Ukweli arusha umeme umekuwa bidhaa adimu sana,uku kata ya sombetini utasema mtoto ndo kakabidhiwa mtambo wa kukatia na kuwasha maana ni kata washa mara mia
 
wameshindwa kazi ?.

ngoja tulete mbadala wao, ....NetGroup Solution kutoka south africa...

c.c. Lowasa.
 
Yaani ni kero balaa, sijui ni mgao au? Yaani hii nchi hapana mi sina tu uwezo wanakera mpaka basi, yaani mpk nadiriki kusema bora alieibua issue ya escrow asingefanya hivyo, wakati wa muhongo hii migawo ya hovyohovyo waliiacha,
 
Back
Top Bottom